MKUU
 wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara ya kushtukiza katika 
masoko manne ya Manispaa ya Moshi pamoja na dampo za kukusanyia uchafu, 
ili kujionea hali ya usafi na utendaji kazi katika mkoa huo. Katika 
ziara hiyo, RC Makalla alitumia muda huo kuwaagiza watendaji wake, 
hususan katika mchakato mzima wa kuifanya Moshi iwe kwenye usafi.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla mwenye miwani, akikagua 
soko lililopo kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya 
ziara ya kushtukiza kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya 
mkoa huo.
Akizungumzia ziara yake hiyo, Makalla alitoa siku tatu kwa 
watendaji wa Manispaa ya Moshi kuhakikisha kwamba lundo la takataka 
katika soko la Kwasadala linaondoshwa haraka iwezekanavyo. Alisema 
hawezi kukubali kuona Manispaa hiyo inashuka kiwango chake cha kuifanya 
Moshi inaendelea kuheshimika katika suala zima la usafi.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla aliyesimama mlangoni, 
akiendelea na ziara yake ya kushtukiza kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani 
Kilimanjaro kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
“Pamoja na kuagiza kuondoshwa kwa uchafu huo, pia nataka kuona 
Mkoa wetu wote unakuwa kwenye hali ya usafi, magari ya usafi yazoe taka 
kwa wakati, uongozi wa masoko uthamini usafi bila kusahau uongozi wa 
Hospitali ya Hai unakamilisha haraka ukarabati wa vyoo,” alisema 
Makalla. Kwa mujibu wa RC Makalla, kitendo cha kuiweka Moshi katika 
mazingira ya uchafu si tu inaondosha kwa kasi ile heshima yake, bali pia
 itazalisha ugonjwa wa mripuko, ukiwamo ule wa Kipindupindu unaosikika 
kuweka katika kambi katika baadhi ya wilaya nchini Tanzania. 
 
 
 
 
 
 


 
 
0 comments:
Post a Comment