Meneja
Chapa (Pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Shomari Shija
(wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani)
wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la
“Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na
utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea
maendeleo binafsi. (katikati) ni Mkuu wa masoko bidhaa za pombe kali za
Diageo-Serengeti Breweries Limited (SBL), Stanley Samtu na kulia ni Dj
maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya
pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.
Mkuu
wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries
Limited(SBL), Stanley Samtu (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie
Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la
kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile
wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. (Kushoto) ni Meneja
Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija na
(kulia) ni Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni
chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
hapa nchini.
Mkuu
wa masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries
Limited(SBL),Stanley Samtu (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie
Walker iliyopewa jina la “Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la
kuhamasisha watu kuwa na utamaduni wa kupenda na kufurahia kile
wanachokifanya katika kujiletea maendeleo binafsi. (Kushoto) ni Meneja
Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija na
(kulia) ni Dj maarufu kutoka Ireland Frank Jez. “Johnnie Walker” ni
chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
hapa nchini.
Mkuu wa
masoko bidhaa za pombe kali za Diageo-Serengeti Breweries Limited (SBL),
Stanley Samtu (kushoto), Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya
Serengeti (SBL) Shomari Shija (kulia) na Dj maarufu kutoka Ireland
Frank Jez (katikati) wakionyesha bidhaa mbalimbali za Johnnie Walker
wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Johnnie Walker iliyopewa jina la
“Furaha itakufikisha mbali” yenye lengo la kuhamasisha watu kuwa na
utamaduni wa kupenda na kufurahia kile wanachokifanya katika kujiletea
maendeleo binafsi. “Johnnie Walker” ni chapa maarufu ya pombe kali
inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchini.
CHAPA
maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
Breweries “Johnnie Walker” imezindua kampeni mpya iliyopewa jina la
“Furaha itakufikisha mbali” siku ya leo katika hoteli ya Serena jijini
Dar es salaam ikiwa na lengo la kuwahamasisha watu kuwa na furaha katika
kila wanachokifanya kwa vile furaha huleta maendeleo na sio kinyume
chake kama wengi wanavyodhani.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa Kampeni hiyo katika hoteli ya
Serena, Mkuu wa kitengo cha Masoko pombe kali wa Kampuni ya bia ya
Serngeti (SBL) Stanley Samtu alisema “Kama chapa, Johnnie Walker
imesimama daima kwenye upande wa maendeleo. Imekuwa hivyo kwa miaka
takribani 200 tangu mwanzilishi Johnnie Walker alipoanza ufundi wake.
Uzoefu
umetufundisha kwamba maendeleo hayatakiwi kuwa safari ya kupanda tu na
isiyo na kikomo bali tunaweza kupiga hatua na kufurahia katika malengo
tunayoweza kuyafikia kila kukicha. Hiyo ndio maana halisi ya kampeni hii
ya Furaha itakufikisha mbali zaidi”.
Kufurahia
kile unachokifanya ni sehemu kubwa na muhimu ya kufanikiwa na kuwa na
maendeleo. Katika juhudi za kufikisha ujumbe kwa wahusika, Johnnie
Walker inategemea kuwamulikia baadhi ya nyota katika fani mbalimbali
waliojizolea umaarufu kutokana na mafanikio walioyafikia. Hawa ni pamoja
na Sheria Ngowi wa tasnia ya mitindo, Dj Frank Jez kutoka Ireland na Dj
Peter Mo. Vijana hawa wote wamebobea katika kile wanachokifanya na
wamekuwa mfano wa kuigwa nchini.
Wamekuwa
sehemu ya dunia ya watu ambao wanaaamini kuwa chanya siku zote katika
kazi ni moja kati ya vitu viliyowasaidia kufika mbele zaidi katika fani
zao.
0 comments:
Post a Comment