Mratibu
 Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la 
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendelea na ukaguzi wa Bwawa hilo.
Wananchi wakiendelea kuchimba bwawa hilo.
Ofisa
 Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas 
(kushoto) akisoma taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali 
inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mkoa wa Tabora. 
Pichani wa pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa 
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez 
pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
 katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maulidah 
Hassan (wa tatu kushoto) wakipitia taarifa hiyo kwa pamoja kabla ya 
kuelekea kukagua miradi hiyo.
MRATIBU
 Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika 
la Mipango ya Maendeleo la Umoja huo Bw.Alvaro Rodriguez, amesema kwamba
 umoja huo utaendelea kufadhili miradi ya maendeleo katika mkoa wa 
Tabora yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi.
Hayo alisema jana baada ya kuzuru miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Tabora.
Miradi
 hiyo ni ya ujenzi wa bwawa la nguvumoja kwamtindo wa utoaji wa chakula 
kwa kazi inayofanywa na mradi wa misitu ya miyombo.
Katika
 ziara hiyo ambayo alikuwa na Ofisa kutoka Kitengo cha ushirikiano wa 
kimataifa wizara ya mambo ya nchi za nje, Bi. Maulidah Hassan Mratibu 
huyo aliridhishwa na mafanikio ya miradi hiyo ambayo imelenga kupiga 
vita umaskini na kutunza mazingira.
Ziara
 ya Mratibu huyo mkoani Tabora ni moja ya ziara yake ndefu ya kutembelea
 miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mikoa ya 
Singida, Tabora na Kigoma.
Alipotoka
 Singida jana asubuhi alifika katika moja ya Wilaya kame nchini, Wilaya 
ya Igunga na kuona mradi unaofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula 
la Umoja wa Mataifa (WFP) wa ukarabati wa bwawa la Charco.
Bwawa
 hilo ambalo litahudumia watu takribani 6,100 kutoka vijiji vya 
Nguvumoja, Ndembezi na Iborogelo lilijengwa awali na miradi ya TASAF 
lakini wakati wa mvua za Elnino tuta lake lilivurugika vibaya.
Akizungumzia
 bwawa hilokaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga ambaye pia ni Ofisa
 Kilimo na Ushirika wa Wilaya ya Igunga, Samaluku Joseas, akizungumza 
alisema kwenye bwawa hilo kwamba Umoja wa Mataifa kupitia WFP 
wanawezesha ukarabati wa bwawa hilo kwa kutoa chakula kwa wachimbaji.
Aidha
 imeelezwa kuwa tuta hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia 
kaya 1,200 na Ng’ombe elfu moja na kuweza kuhifadhi maji kwa mwaka 
mzima.Imeelezwa
 kuwa wajenzi wanapewa debe moja la Mahindi kwa kina cha mita moja na 
urefu wa mita nne na upana wa mita tatu na nusu lita ya mafuta ya kula 
na Njegere kilo tatu.Kumalizika kwa bwawa hilo kutasaidia kupunguza umbali wa wananchi katika kutafuta maji.
Awali
 wananchi walilazimika kusafiri kilomita 30 kupata maji katika bwawa la 
Manzugi kuchota maji na kunywesha mifugo.Aidha imeelezwa kuwa baadae 
wanyama watatengewa eneo la kunywa maji.
Aidha
 alitembelea kikundi cha ufugaji nyuki, utunzaji wa mazingira pamoja na 
usindikaji wa matunda pori cha Membo , wilayani Uyui.
Kikundi
 hicho kilichopo wilayani Uyui kimeanzishwa Mei 8,2007 na Katibu wa 
kikundi Nasibu Baraka alisema kikundi hicho chenye wanachama 30 
kimefanyakazi kubwa ya kupiga vita umaskini.Alisema
 ili kukabiliana na adui njaa na umaskini kikundi hicho kwa ufadhili wa 
UNDP kimewezesha kujiajiri wenyewe, Kusindika matunda ya asili kwa ajili
 ya jamu na divai,kilimo cha bustani, kilimo cha chakula na biashara, 
ujenzi wa majikobanifu,usagaji wa unga na kupika keki za Muhogo mbichi 
kwa Karanga na Asali.
Akisoma
 risala kwa Mratibu wa UN Tanzania alisema kwamba wamekuwa na mafanikio 
makubwa kutokana na ruzuku mbalimbali za UNDP ikiwamo mafunzo.
Aidha
 amesema kwamba kwa sasa wanatumia sola badala ya mafuta ya taa huku 
mradi wa Miyombo ukiendelea kuleta neema.Aidha ametaka umoja huo 
kuwasaidia kuwa na mshine za kisasa cha kusindika matunda na chakula.
Viongozi
 hao walifika katika mradi huo kuangalia mafanikio ya mradi huo 
unaotekelezwa chini ya mpango wa miaka mitano wa Msaada wa Maendeleo wa 
Umoja wa Mataifa,(UNDAP).Aidha
 mradi huo umelenga kupunguza umaskini kutunza mazingira kwa njia ya 
uragibishi na na kufunza wananchi kuhusu suala la ufugaji nyuki na 
utunzaji wa mazingira.
Naye 
Ofisa utawala msaidizi wa mkoa anayeshughulikia Uchumi na Tija Dk. 
Phillips Mtiba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Tabora, Ludovick 
Mwananzila ambaye hakuwepo kutokana na majukumu mengine kwenye mikutano 
na wananchi kuhusu miradi ya TASAF, alisema baada ya kumaliza kukagua 
miradi kwamba wameridhika na miradi inayofadhiliwa na UN katika mkoa 
huo.
Alisema
 pamoja na kwamba walitembelea miradi michache lakini ni dhahiri mkoa wa
 Tabora umefurahishwa na misaada iliyotolewa ambayo inatia moyo na 
kusaidia harakati za serikali za kukomboa wananchi wake kutoka katika 
lindi la umaskini na ukosefu wa huduma muhimu kama za maji na hifadhi ya
 mazingira.
Pamoja
 na kushukuru kwa misaada hiyo kwa wanatabora na maendeleo yao, alitaka 
UN isiwachoke kusaidia vipaumbele vya mkoa huo ambavyo ni kujitokeza kwa
 chakula na hifadhi ya misitu.“ 
Nashukuru sana kwa msaada tunaoendelea kupata kutoka UN kwa ajili ya 
maendeleo ya wana Tabora na Tabora kwa ujumla na niseme tu kwamba kama 
wana Tabora kuna vitu ambavyo tunaweza kufanya na mengine hatuwezi 
kuyafanya na hapo ndipo sasa tunapoweza kuona umuhimu wa nafasi ya 
wafadhili na wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo.” Alisema Dk.
 Phillips.
Alisema
 ingawa walikuwa na muda mfupi na kutembelea miradi michache , alitamani
 waje kurudi kuona miradi mingi zaidi ili watambue kwamba miradi hiyo 
inabadilisha wana Tabora na hawachezei fedha za ufadhili.
Alisema
 suala la uhakika wa chakula kwa wananchi ni muhimu kwao kutokana na 
ukweli kuwa wananchi wakiwa na chakula hata fedha zao zitakaa mfukoni na
 kufanya kazi nyingine za maendeleo. Alisema kutokana na hali hiyo 
wataendelea kuomba kusaidiwa katika eneo hilo.
Aidha
 alitaka mkoa wa Tabora kuendelea kusaidiwa kutunza misitu ya Miyombo 
kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa misitu ni 
kivuta mvua na maji ndio pembejeo namba moja katika uzalishaji wa 
chakula.
Alishukuru
 UNDP kwa kusaidia kuhifadhi misitu hiyo ili kuwapo na uvunaji endelevu 
kwa kusaidia jamii kuitunza na kuismamia rasilimali hiyo na kuitumia 
katika fursa za kiuchumi kama ufugaji nyuki.
Leo Mratibu huyo ataendelea na ziara yake katika mkoa wa Kigoma.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment