Gari
la Kuzoa taka kutoka katika Manispaa ya Kinondoni likiwa limebeba taka
kutoka Soko la Tandale tayari kwenda kuzihifadhi katika dampo kuu,
Manispaa hiyo imekuwa ikihakikisha hali ya usafi katika masoko yake kwa
kupeleka magari ya kuzoa taka kila siku ili kuepukana na magonjwa
ambukizi ikiwemo kipindupindu.
Sehemu ya Soko lilipo kwenye kituo cha Daladala cha Simu 2000 eneo la
Sinza kikiwa katika hali nzuri ya usafi huku uongozi wa eneo hilo
wakiendelea kuisimamia hali hiyo kama ambavyo ilivyoagizwa na Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuwa siku
ya sherehe ya Uhuru ambayo huadhimishwa kila Desemba 9, mwezi wa 12 kuwa
ni siku ya usafi wa mazingira ili kuepukana na magonjwa amukizi
kikiwemo kipindupindu.
Sehemu
ya Daraja la Tegeta Manispaa ya Kinondoni ikiwa imegeuzwa Dampo na
wakazi wa eneo hilo kwa ambapo Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa
Dodoma Bi.Susano Chekani aliagiza uchafu huo kutolewa haraka kwa kuwa
inahatarisha hali ya afya kwa wakazi wa maeneo hayo .
Wajumbe
wa mkutano wa usafi ambao pia ni wadau kutoka taasisi mbalimbali
zikiwemo Taasisi za kifedha, Mazingira,Jeshi la
Magereza,Wanamazingira,Vikundi vya Usafi na Wafanyakazi wa Manispaa ya
Kinondoni wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo
ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya sikuu ya Uhuru, Desemba 9
mwaka huu kuwa siku ya kufanya usafi .

Mkurugenzi
wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akikagua Soko la
Magomeni lilipo Manispaa ya Kinondoni wakati ziara ya kuangalia hali ya
usafi ikiwa ni kutekeleza agizo lililotolewa na Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli kuadhimisha siku ya
sikuu ya Uhuru, Desemba 9 kuwa siku ya kufanya usafi,kulia kwake ni
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Injinia Mussa Natty.
Mkurugenzi
wa Idara ya Tawala za Mikoa Dodoma Bi.Susano Chekani akiongea na
wachuuzi wa Soko la Magomeni katika Manispaa ya Kinondoni katika ziara
ya kuangalia hali ya usafi katika soko hilo.
0 comments:
Post a Comment