Mshitakiwa
 namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, Tiagi Masamaki (katikati) na
 washitakiwa wenzake wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es 
Salaam leo mchana baada ya kusomewa mashitaka yao.
MAOFISA wanane wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwemo Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo Tiagi Masamaki (56) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7 za kitanzania.
Ukimuondoa
 Masamaki maofisa wengine waliopandishwa kortini ni Habibu Mponezya (45)
 Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja,Bulton Mponezya (51) 
Wakili
 wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa akisaidiana na Peter Vitalis 
ameadi leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya 
Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa 
makosa mawili.
Alidai
 makosa mawili ya uhujumu uchumi ni kula njama ya kuidanganya Serikali 
na kuisababishia Serikali hasara. Kesi hiyo ni namba 35/2015 ya uhujumu 
uchumi. 
Ilidaiwa
 katika shtaka la kwanza katika tarehe tofauti kati ya Juni 1 na Novemba
 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa 
pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa sh. bilioni 12.7 
zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika Bandari Kavu ya Azam, baada ya
 kodi zote kutolewa.
Katika
 shtaka la pili, washtakiwa wanatuhumiwa katika ya Juni Mosi na Novemba 
17 mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam walishindwa kutimiza 
majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata 
hasara ya sh. bilioni 12.7.
Baada
 ya washtakiwa hao kusomewa makosa yao, Hakimu Shahidi aliwaeleza kuwa 
mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo hawatakiwi
 kujibu chochote kama kweli au si kweli.
Aliongeza
 kuwa Mahakama Kuu ndiyo inamamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kwa hiyo 
kama wanataka dhamana wapeleke maombi ya dhamana katika mahakama hiyo.
"Kama mnataka dhamana pelekeni maombi Mahakama Kuu kwa sababu mahakama hii hawezi kutoa dhamana," alisema Hakimu Shahidi 
Hata
 hivyo, upande wa utetezi ulidai kuwa kesi hiyo ifikishwa mahakamani 
hapo bila kibali na pia waliomba mshtakiwa namba nne Mrema anamtoto 
mchanga kwa hiyo wanaiomba mahakama imfikirie.
Wakili
 Msigwa alidai upelelezi bado unaendelea, wanaomba tarehe nyingine ya 
kutajwa. Kesi hiyo itatajwa Desemba 17 mwaka huu kuangalia kama 
upelelezi utakuwa umekamilika
Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment