Kamishna
 Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akiwasilia katiki viwanja vya 
Magereza Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya hafla ya kukabishi bendera kwa
 watumishi 39 wa Jehi hilo wanaotarajia kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa
 Tanganyika kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.
Kamishna
 Jenerali wa Magereza John Minja akikabidhi bendera ya Magereza kwa 
kiongozi wa Msafara Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy leo 
tarehe 04/12/2015 wakiwa wanajiandaa kupanda Mlima tarehe 06/12/2015 ili
 ifikapo tarehe 09 siku ya Uhuru wa Tanganyika wawe kileleni
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza John Minja akitoa nasaha kwa wapanda mlima wa Jeshi la Magereza (Hawapo pichani)
Baadhi
 ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima 
Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini nasaha za Kamishna Jenerali wa 
Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa bendera ya Jeshi hilo 
kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.
Baadhi
 ya wadau wa Magereza Utalii Klabu walio tayari kupanda Mlima 
Kilimanjaro wakiimba nyimbo za hamasa baada ya kupokea bendera kutoka 
kwa Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja katika hafla ya kukabidhiwa
 bendera ya Jeshi hilo kuipeleka katika Kilele cha Mlima huo.
Wapanda
 Mlima Kilimanjaro wa Jeshi la Magereza wakiwa katika picha ya pamoja na
 Mkuu wa Jeshi la Magereza John Minja (Katikati),wa tatu kulia ni Mkuu 
wa Magereza Mkoa wa Arusha SACP Hamis Nkubasi, na Mkuu wa Magereza Mkoa 
wa Kilimanjaro SACP Venant Kayombo, wa tatu kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa 
Magereza Mkoa
Wadau
 wa Magereza Utalii Klabu wakiwa katika mazoezi mbalimbali ya kukimbia 
na kutembea katika viunga vya mji wa Moshi ikiwa ni maandalizi ya 
kuelekea katika kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya 
kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika sambamba na kuamasisha 
utalii wa ndani.
Picha zote na Mrakibu Msaidizi wa Magereza Deodatus Kazinja na Koplo Mfaume Abdalah wa Jeshi la Magereza
……………………………………………………………………………………………..
Na Deodatus Kazinja
Katika kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika tarehe 9 
Desemba watumishi wapatao 39 Jeshi la Magereza wakiwa katika uwiano wa 
wanaume 30 na wanawake 9 wataadhimisha siku hiyo kwa kupanda mlima 
Kilimanjaro na kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.
 
Washiriki hawa wanatoka katika vituo vya Makao Makuu ya 
Magereza, Chuo cha Taaluma ya urekebishaji Ukonga Dar es salaam, Kikosi 
Maalum cha Kutuliza Gasia Magereza (KMKGM), Pwani, Dar es salaam, 
Iringa, Mbeya, Mara, Tabora, Tanga, Kilimanjaro na Arusha ambao kwa 
gharama zao wameamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa 
kufanya utalii wa ndani.
 
Akiongea na waandishi wa habari Kamishna Jenerali wa Magereza 
nchini John Casmir Minja katika hafula fupi ya kuwakabidhi bendera 
watumishi hao katika viwanja vya Magereza Mkoa wa Kilimanjaro amesema 
amefurahishwa mno na uamuzi wa askari hao kwa vile unalitangaza Jeshi la
 Magereza nje ya mipaka yake.Kamishna Minja alisema pia mbali na kulitangaza Jeshi la 
Magereza unawaweka timamu watumishi hao katika kufanya kazi zao vizuri 
ikiwa ni kuunga kauli mbiu ya serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi tu.
 
Aidha Kamishna huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru serikali kwa 
namna ambavyo imekuwa ikijitolea kulisaidia Jeshi la Magereza ambapo 
alitoa taarifa kuwa tayari mikataba ya kununuliwa magari yapatayo 905 na
 ujenzi wa nyumba za watumishi zipatazo 9500 imesainiwa na magari 
yataanza kuingia mapema Januari 2016.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa Magereza Utalii Klabu ambaye pia 
ni Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Ndugu Estomih Hamis mbali na 
kumshuruku Kamishna Minja akwa namna ambavyo amejitolea katika 
kufanikisha uanzishwaji wa Klabu hiyo kuelezea dhima nzima ya utalii 
huo.
 
 “ Tumeamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa 
mfumo huu kwa sababu kadhaa. Mosi , ni kuunga mkono jitihada za serikali
 za muda mrefu za kuhamasisha utalii wa ndani ambacho ni chanzo 
kimojawapo cha kuongeza mapato ya ndani ya serikali”
“Pili, ni kuleta mwamko kwa watumishi wa umma na watanzania kwa 
ujumla katika kutembelea vivutio vya utalii vya ndani kuliko ilivyo sasa
 ambapo sehemu kubwa ya watalii ni wageni kutoka nje ya Tanzania”
 
Aidha, ndugu Hamis aliongeza kuwa zoezi la upandaji mlima 
Kilimanjaro ni zuri kwa kuimarisha afya za watumishi hivyo kujiepusha na
 magonjwa kama vile kisukari, shinikizo la damu na utimamu wa mwili na 
hasa kwa askari wanaotakiwa kuwa hivyo muda wote.
Tukio la watumishi wa Magereza kupanda mlima Kilimanjaro 
litakuwa ni la pili kwa mwaka huu ambapo mara ya mwisho walipanda mlima 
tarehe 6 March, 2015 wakiwa ni jumla ya watumishi 20 ambapo 16 
walifanikiwa kufika kileleni na wanne kurudia njiani kwa sababu 
mbalimbali.
 
Zoezi la upandaji mlima lililopita lilifanyika kwa mafanikio 
makubwa kiasi cha kuibua hoja y wa unndwaji wa chombo cha pamoja 
kinachoweza kuratibu shughuli za utalii ndani ya Jeshi la Magereza kwa 
kuwaunganisha watumishi wote.
 
Hoja hiyo ilifanikiwa kwa kuundwa kwa Klabu ya Utalii ya 
Magereza, klabu ambayo iko katika hatua za mwisho za usajili. Tayari 
Klabu hiyo inao viongozi wakiongozwa na Mwenyikiti ndugu Hamis, katibu 
wake akiwa ni Mkaguzi wa Magereza Dominick Mshana na Mweka Hazina ni 
Mrakibu Msaidizi wa Magereza Erasto Kipingu.
Nani analipa gharama za utalii huo?
 
Akijibu swali hilo katibu wa Klabu hiyo Mkaguzi Mshana alisema 
kwa hivi sasa watumishi hao wanapanda kwa gharama zao wenyewe kutoka 
katika mishahara yao ambapo karibu kila mshiriki amechanga wastani wa 
shilingi 300,000.Mshana amesema ni matumaini yake kuwa katika siku za mbeleni 
kama watapatikana wadhamini gharama hizo zinaweza kupungua sana kutoka 
mifukoni mwa washiri. 
 
Aidha amesema gharama za kupanda mlima na kutembelea vivutio 
vingine kwa ujumla ni kubwa kwa mtu mmoja mmoja lakini kunakuwa na 
unafuu mkubwa watu wakipanda kama kikundi.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment