Afisa
Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki (kushoto) na Meneja uhusiano wa
Airtel, Jackson Mmbando (katikati) wakipima uzito wa kuku wa kienyeji
wanaofugwa kisasa na kijana Mohamed Kigumi (kulia), anayeishi Kiluvyia
jijini Dar Es Salaam baada baada ya kutembelewa nyumbani kwao na kuona
maendeleo aliyoyapata baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wa
Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ miezi sita iliyopita.
Afisa
Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) na Meneja uhusiano wa Airtel,
Jackson Mmbando (katikati) wakitazama maandalizi ya utunzaji wa kuku wa
kienyeji wanaofugwa kisasa na kijana Mohamed Kigumi (kulia), anayeishi
Kiluvyia jijini Dar Es Salaam baada baada ya kutembelewa nyumbani kwao
na kuona maendeleo aliyoyapata baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia
mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ miezi sita iliyopita.
Kijana
Mohamed Kigumi anayeishi Kiluvyia jijini Dar Es Salaam akiwaelekeza
meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (katikati) na afisa Uhusiano
wa Airtel, jinsi anavyoendesha ufugaji wake wa kuku baada ya kumtembelea
nyumbani kwao na kuona maendeleo aliyoyapata baada ya kuwezeshwa na
Airtel kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ miezi sita
iliyopita.
VIJANA
wengi wana ndoto za kujiletea maendeleo lakini wanashindwa kutimiza
ndoto zao kutokana na kukosa elimu sahihi na kutokuwa na mitaji ambayo
ingewawezesha kujiunga kwenye miradi ya ujasiriamali.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA imeiona
changamoto hiyo na kuamua kuwafikia vijana mbali mbali hapa nchini
akiwemo kijana Mohamed Kigumi ambaye mpaka sasa ameonesha jitihada za
kujikwamua na umaskini kwa kuwawezesha kupata mitaji ama vifaa
vitakavyotimiza ndoto zao.
Akiongea
katika kijiji cha kiluvya, Muhamed Kigumi ambaye anajishuhulisha na
ufugaji wa kuku wa kienyeji, amesema licha ya kuanza kazi hiyo kwa muda
mrefu lakini sasa ameanza kuona mafanikio makubwa katika kazi yake
kutokana na kujengewa mabanda ya kisasa ya kufugia kuku wake na mfuko wa
Airtel FURSA tofauti na hapo awali ambapo alikuwa akifugia kukuwake
kwenye mazingira magumu.
Amesema
mabanda ya kisasa aliyojengewa na mfuko wa Airtel FURSA pamoja na
kupatiwa msaada wa kuku, maisha yake yamebadilika kwani sasa ameamua
kujiajiri katika kazi hiyo na kumuwezesha kusaidia familia na kuuomba
mfuko huo kendelea kuwasaidia vijana wengine hapa nchini.
Akiongea
katika mabanda ya kuku ya kijana huyo alipomtembelea hapo jana, meneja
uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema kuwa mpango wao wa Airtel
FURSA umefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo wamemtembelea bila
kumpa taarifa lakini wamebaini kuwa msaada waliompatia kijana Mohamed
umeweza kuyabadilisha maisha yake kutokana na kuwa makini na kazi yake.
Mmbando
aliongeza kwa kusema, mpango wa kuwasaidia vijana wenye umri kati ya
miaka 18-24 uitwao Airtel FURSA umeanzishwa na mtandao wa simu za
mikononi wa Airtel ili kuwasaidia vijana wa Tanzania wenye ndoto zao ili
kuweza kuzitimiza ndoto zao kwa kuwawezesha kwa kuwapatia elimu ya
biashara na nyenzo za kufanyia kazi.
0 comments:
Post a Comment