Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo katika 
Ubalozi wa Ufaransa nchini kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 
vilivyotokana na mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Balozi wa Ufaransa nchini 
Tanzania Malika Berak kufuatia vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na 
mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa 
nchini Malika Berak Tanzania mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo
 na kutoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois 
Hollande kufuatia vifo vifo vya Watu zaidi 130 vilivyotokana na 
mashambulizi ya kigaidi.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa pili akiwa katika picha ya pamoja 
na Balozi wa Ufaransa (kushoto) pamoja na Maofisa mbalimbali wa Ubalozi 
huo mara baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ufaransa nchini 
Tanzania Malika Berak mara baada ya kusaini kitabu cha Maombolezo 
Ubalozini hapo.
………………………………………………………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dokta John Pombe Magufuli amesaini kitabu cha Maombolezo katika
 Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es salaam kufuatia vifo vya watu zaidi 
130 vilivyotokea November 15, 2015 kutokana na mashambulizi ya ugaidi 
mjini Paris, Ufaransa.
 
Pamoja na kutia saini kitabu cha maombolezo, Mheshimiwa Dr. 
Magufuli ametoa salamu za pole kwa Rais wa Ufaransa Mheshimiwa Francois 
Hollande na kumuombea uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki 
kigumu Dokta Magufuli ambaye amepokelewa na Balozi wa Ufaransa hapa 
Nchini Bibi Malika Berak amesema Tanzania imeguswa na vifo hivyo na 
inaungana na Ufaransa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
 
Aidha Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wa tukio hilo 
wapone haraka ili waweze kuungan a na familia zao na kuendelea na 
shughuli zao za kila siku Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
Dokta John Pombe Magufuli amewasili Mjini Dodoma jioni hii kwa shughuli 
mbalimbali za kikazi.
 
Mheshimiwa Magufuli amesafiri kwa gari kutoka Dar es salaam hadi
 Dodoma na taarifa ya shughuli atakazozifanya mtaarifiwa baadaye.
Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
November 17, 2015
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment