Mkurugenzi
 wa Uchaguzi wa  NEC Bw. Kailima Ramadhani                           
akizugumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya  viti maalumu 
vya Udiwani ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo  ni viti 
1393, kutoka katika Vyama vya CCM,CHADEMA,NSSR-MAGEUZI pamoja na 
CUF.Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam ,Kulia ni Kaimu 
Mkurugenzi Huduma za Sheria wa NEC Emmanuel Kawishe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uchaguzi wa  NEC Bw. Kailima Ramadhani
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
TUME 
ya Taifa ya Uchaguzi( NEC) imesema hadi sasa viti maalumu vya Udiwani 
ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo  ni viti 1393, kutoka 
katika Vyama vya CCM, CHADEMA, NSSR- MAGEUZI  pamoja na CUF.
Hayo 
yamesemwa leo Jijijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka 
NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa  taarifa kwa Umma kuhusu uteuzi 
wa madiwani wanawake wa Viti Maalumu.
Aidha 
Bw.Ramadhani amesema kuwa idadi ya Viti maalumu Vya Udiwani ni  1,408 
nakwamba kutokana na majimbo nane na kata thelathini na Nne ambapo 
 Uchaguzi haujakamilika kwa Sababu mbalimbali, hatua hiyo itasababisha 
kubakia viti 15 ambavyo vitagawanywa mara baada ya Uchaguzi kukamilika 
ili kufikia idadi ya viti 1,408 kutoka viti 1393 vinavyo tambulika kwa 
sasa.
Aidha 
amefafanua kuwa kutokana na Viti hivyo  Maalumu Vya Udiwani 
Vilivyoteuliwa  na NEC, Chama Cha Mapinduzi CCM kimepata viti 
1,022,Chama Cha Demokrasia na Mawendeleo CHADEMA 280,Chama Cha Wananchi 
CUF-79, ACT WAZALENDO viti 6 pamoja na NSSR  MAGEUZI viti 6.
Amesema
 kuwa tume imeamua kutoa taarifa ya uteuzi wa  viti maalumu Vya Udiwani 
Nchi nzima ya Madiwani waliyoteuliwa na Tume  kutokana na Kanuni za 
Kudumu za Mikutano ya Halmashauri, Mabaraza ya Madiwani yanatakiwa 
kuitishwa siku thelathini tangu tarehe ya Uchaguzi ifanyike.
Katika
 hatua Nyingine Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi  NEC amesema kuwa  mwisho wa
 Uchaguzi katika Majimbo na Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi ni Desemba 
20 mwaka huu, ambapo katika jimbo la Uranga Mashariki pamoja na Lushoto 
uchaguzi utafanyika Novemba 22 mwaka huu,nakuwaomba  Wananchi kujitokeza
 kwa wingi kupiga kura ili kuchagua kiongozi wanaomtaka.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment