Pages

Ads 468x60px

Friday, December 18, 2015

WAZIRI KITWANGA ALA KIAPO CHA KUWA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA 75

75
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta.
76
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.
77
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya kumuapisha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.

0 comments:

Post a Comment

 
Blogger Templates