Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akipokea taarifa ya
makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na
Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid wakati
wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akimsikiliza aliyekuwa
Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya
Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid wakati wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo
jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa
Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt.
Seif Rashid (kushoto) akisalimiana na Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangala (kulia) leo
jijini Dar es salaam.
………………………………………
NA Eleuteri Mangi-MAELEZO
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amekabidhiwa rasmi ofisi na
aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya
Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid leo jijini Dar es salaam.Akipokea ofisi hiyo, Waziri Ummy
alimshukuru Dkt. Seif kwa jitihada kubwa waliyofanya ya kupambana na
magonjwa kwa wananchi na kufanikisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi
duniani ambayo imetatua tatizo la ugonjwa wa polio na kuwa “polio free”..
Aidha, Waziri Ummy amemhakikishia
Dkt Seif kuendelea kushirikiana naye pale msaada wake utakapohitajika
kwa kuwa anauzoefu katika masuala ya afya ili kuwahudumia Watanzania na
kupambana na adui wa taifa ambaye ni magonjwa.Akikabidhi ofisi, Dkt Seif
aliwapongeza Waziri Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Hamisi Kigwangalla
kwa kupewa nyadhifa hizo na kuahidi kuwapa ushirikiano wake
paleutakapohitajika.
Dhana ya “Hapa Kazi Tu” imechukua
mkondo wake ambapo hadi sasa Mwaziri na Manaibu waziri wanatekeleza
dhana hiyo kwa vitendo na siyo kukaa ofisini, kwa kwa juhudi hizo
viongozi kwa kushirikiana na wananchi, Tanzania itafanikiwa kufikia
uchumi wa kati ifikapo 2025 ikiwa na watu wenye afya bora inayowaruhusu
kufanyakazi kwa juhudi na maarifa ili kuwa maendeleo yenye tija kwa
Wtanzania.
0 comments:
Post a Comment