Ni majira
ya saa 10 na dakika 10 Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo
ndipo alipofika katika mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya Tegeta
jijini Dar es Salaam kinachomilikiwa na Tanesco bila ya kutoa taarifa na
kukuta wafanyakazi pamoja na wahandisi wa kituo hicho cha umeme
wakiendelea na kazi katika mitambo hiyo.
Na kukagua
mitambo hiyo leo na kubaini kuwa umeme uniti moja inatengenezwa kwa
gharama ya shilingi 90 na kuuzwa kwa wananchi kwa shilingi 180 ikiwa ni
kiwango kikubwa kwa mwananchi wa kawaida.
Pia Mhongo amesisitiza kuwa umeme unatakiwa kushuka bei ili kila mwananchi anufaike na umeme hapa nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipokea vifaa vya
kuzuia kusikia sauti kuingia masikioni mara baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza katika Mitambo ya Gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akizungumza na Meneja
wa Mitambo ya gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam, Mohamed Kisiwa mara
baada waziri wa Nishati na Madini kutembelea mitambo ya umeme wa gesi wa
Tegeta jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na
Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa mara baada ya waziri
huyo kutembelea mtambo huo bila kutoa taarifa na kuhoji baadhi ya
matengenezo katika mtambo huo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akitembezwa na Meneja
wa Mitambo ya gesi ya Tegeta Mohamed Kisiwa mara baada ya kutembelea
mitambo ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Mitambo ya Gesi iliyotembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na
Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa jijini Dar es Salaam
leo.
0 comments:
Post a Comment