Kwenye list ya mastaa ambao wamejitosa kwenye Siasa 2015, Baba Levo nae yumo… Baba Levo ameshukuru
sana kwa ushindi wake huku akisema kwamba japo kashinda na anakuwa
Diwani Kigoma mjini kwa miaka mitano lakini muziki hatouacha na
atajitahidi pia kusaidia vijana wenye vipaji Kigoma ili waweze
kutambulika kwa sanaa wanazofanya.
Kingwendu
nae aliingia kwenye Siasa japo Kura hazikutosha hivyo kashindwa kuibuka
na ushindi, amesema kushindwa kwake kunafanya ajipange upya kwa ajili
Siasa kwenye msimu mwingine wa Uchaguzi 2020 Tanzania.
Account ya Instagram ya staa wa Big Brother, Idris Sultan
haiko hewani… kama ulishtuka kutokumuona upande huo basi taarifa
ikufikie kwamba Wamiliki wa Mtandao wa Instagram wameifungia account
yake kwa muda kwa sababu alikiuka kanuni za Mtandao huo.
Idris amesema alifungiwa baada ya kupost kipande cha video kutoka kwenye movie ambacho yeye hakujua kwamba hiyo movie imefungiwa… Idris amesema yuko kwenye mipango ya kujadiliana na Wamiliki wa Mtandao huo ili wamfungulie.
0 comments:
Post a Comment