Muigizaji Kingwendu ni miongoni mwa mastaa ambao wamechukua headline za kugombea Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kama Afande Sele, Professor Jay, Muigizaji Frank na wengineo.
Stori iliyonifikia ni kwamba muigizaji 
huyo hakufanikiwa kupata Ubunge kupitia tiketi ya CUF katika  jimbo la 
Kisarawe mkoa wa Pwani.
Akiongea na ripota wa millardayo.com alisema…’Matokeo ya mwanzo yalikuwa yanaonesha kwamba mimi naongoza, lakini mwishoni katika hesabu ikaonekana amenishinda‘- KINGWENDU
‘Matokeo 
yanaonesha Suleimani Jako wa CCM ameshinda, nimejaribu na nimethubutu 
kwa mara ya kwanza..! najua nimekosea wapi na ntajipanga upya na ntaenda
 kusomea siasa zaidi’– KINGWENDU
‘Hakuna 
mtu aliyenishawishi kugombea ubunge, bali ni mimi mwenyewe niliamua 
baada ya kuona pia baadhi ya wasanii wenzangu wanagombania‘-KINGWENDU
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment