Agizo la Rais Magufuli la
kupatikana kwa mashine mpya ya CT Scan katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili limeonekana kuzaa matunda baada ya Serikali kununua mashine
mpya ambayo imegharimu dola za Kimarekani milioni 1.7.
Kutokana na mashine ya awali kuhabikika kila wakati Serikali imegharamia mashine mpya ambayo imeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi tofauti na nyingine zilizowahi kutumiwa na hospitali hiyo.
Neema Mwangoko ambaye ni afisa Uhusiano wa hospitali hiyo amesema mashine hiyo mpya ina siku tatu tangu ifungwe na tayari imehudumia wagonjwa 26 mpaka sasa na bado ipo kwenye majaribio.
Naibu waziri wa afya Dk.Hamis Kigwangala ambaye alifanya ziara katika hospitali hiyo amepongeza hatua hiyo na kutaka watendaji waboreshe huduma zinazotolewa na hospitali hiyo kwa wateja wake.

0 comments:
Post a Comment