Wananchi
wa Mkoa wa Geita wameaswa kufuata kanuni za usafi wa mazingira ili
kudhibiti maumbukizi ya ugonjwa wa kipindupindu,Hayo yamesemwa leo na
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu
mara baada ya kutembelea kambi ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha
afya cha Nyankumbu,mkoani hapa
Waziri
Ummy akivaa vifaa maalum vya kujikinga na kipindupindu kabla ya kuingia
kwenye kambi hiyo,kulia ni Mganga mfawidhi wa Kituo hicho Josephat
Msafiri.(Picha Zote na Catherine Sungura WAMJW-GEITA)
Waziri Ummy akivua vifaa hivyo mara baada ya kutoka kuwasalimia wagonjwa
wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo,wagonjwa waliopo hadi leo
mchana ni wagonjwa wanne
Waziri huyo akiongea na mmoja wa wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi hiyo
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiwasalimia wagonjwa wa kipindupindu(hawapo pichani)kulia ni Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt.Joseph Kisala
Baadhi ya wagonjwa wa kipindupindu waliolazwa kwenye kambi ya kituo cha afya cha Nyankumbu
0 comments:
Post a Comment