Afisa 
Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini 
Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha 
shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
 na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika
 ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Afisa 
Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini 
Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akimwonyesha Naibu Waziri wa Afya, 
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla 
moja ya damu ambayo ni maalum kwa wamama wajawazito wakati wa kujifungua
 zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika mabara hiyo.
Mmoja 
wa watumishi katika maabara ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama 
(ambaye jina lake halipatikana) akiendelea kutekeleza majukumu yake kama
 alivyokutwa na mpiga picha wetu.
Na Modewjiblog, Team.
Naibu
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. 
Hamisi Kigwangalla ameagiza watanzania wote wasikubali kutozwa rushwa 
kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo 
watamchukulia hatua kali.
Kauli
 hiyo imetolewa mapema Januari 4 (jana) na Naibu huyo wa Waziri wa Afya,
 Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Kingwangalla 
alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo
 jijini Dares Salaam.
Dk.
 Kigwangalla amefafanua kuwa, kwa watu wote ikiwemo Nesi, Daktari ama 
mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo
 kufukuzwa kazi.“Kwa
 watanzania wote, msikubali kutoa rushwa kwa ajili ya damu. Na kama 
itatokea Nesi ama Daktari ama nani, anakuambia ulipie ili upate damu!. 
Kwa sababu kuna uhaba wa damu kwa sasa.. Ripoti kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu
 wa Mkoa ama Daktari Mkuu husika ama fika Wizara ya afya moja kwa moja 
na kuna namba tutaitoa kwa watanzania wote mtupatie ripoti.
Mtu
 atakayekutoza damu, wewe tuambie, huyo tutamfukuza kazi moja kwa moja, 
hatuwezi kuendekeza watu wa namna hii... Serikali inaingia gharama kubwa
 kukusanya damu kwa watu, Kuna watu wanajitolea damu zao bure. Leo wewe 
nesi ama mganga ukauze damu, hilo jambo hatutakubali hata kidogo kwa 
hiyo natoa rai kwa watanzaia hiyo damu ni bure na haiuzwi na usikubali 
kuuziwa damu hata kidogo.” Ameeleza hilo Dk. Kigwangalla.
Awali
 katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameipongeza Ofisi ya Mpango wa Taifa
 wa Damu Salama kwa kazi wanayofanya na ubunifu waliofikia wa kuhusisha 
Halmshauri katika ukusanyaji wa damu huku wao wakisimamia kudhibiti 
viwango vya damu ya matumizi kwa watanzania huku akitumia wasaha huo 
kutoa maelekezo ya kuboresha mfumo wa motisha kwa wanaochangia damu 
salama ambapo kwa wachangiaji damu kuingizwa kwenye mfumo wa 
kieletroniki wa kuwatambua watu wanaochangia damu, kutoa taarifa jinsi 
damu zao zilivyookoa miasha ya wagonjwa na kuwapa motisha ili waweze 
kuwa wachangiaji endelevu.
“Motisha
 sio soda na maji kwa wanaochangia damu. Motisha ni hata kupewa taarifa 
kwamba damu yake imesaidia kuokoa maisha ya mwanadamu mwenzake aliyekuwa
 anaumwa ugonjwa fulani, hii ni motisha kubwa sana kuliko hata pesa, ama
 soda ama maji yanayotolewa anapochangia damu.
Lakini
 kama imeshajitokeza mtu kuwa na tabia ya kuchangia damu, huyu sio wa 
kumpoteza, maana yake kuna uwezekano mkubwa wa akarudi tena kuchangia 
damu, mtu huyu ni lazima kuwe na mfumo wa kielekrioniki wa komputa wa 
kumtakia salamu, taarifa na anakuwa kwenye database yenu.
“Mnatakiwa
 muwe na mfumo wa kumpa taarifa pindi damu yake imetumika, ikiwemo 
kumueleza kuwa damu yako imemsaidia Mama mjamzito aliyejifungua na 
kutokwa damu nyingi, na mtu huyo akipata taarifa hiyo ni motisha tosha 
hivyo ni lazima muwe na huo mfumo kutoa motisha zaidi.
Naibu 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
 Kingwangalla na msafara wake wakishuka ngazi kuelekea kukagua idara 
mbalimbali katika ofisi hizo, Januari 4, 2016.
Awali
 akielezwa na Meneja wa kanda ya Mashariki katika Ofisi za Mpango wa 
Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa 
kwamba changamoto zilizopo katika upatikanaji wa damu nchini ni 
halimshauri kutenga bajeti za kutosha kwa ajili ya huduma hiyo, Kwa 
hatua hiyo, Dk. Kigwangalla ameziagiza Halmshauri zote nchini 
kuhakikisha zinatenga bajeti za kutosha ilikusapoti mpango wa damu 
salama.
Katika
 hilo Dk. Kigwangalla ameapa kuwashughulikia wale wote watakaozembea na 
kuwachukulia hatua kali Ma DMO, Wakurugenzi na kushtakiwa kwa mamlaka 
zilizopo na kufukuzwa kazi.
“Naziagiza
 Halmashauri zote kuhakikisha zinatenga bajeti za kusapoti mpango wa 
ukusanyaji damu salama. Na Halmashauri zitakazoshindwa, DMO na 
Mkurugenzi wake tutahakikisha tunawashtaki kwa mamlaka zilizowateua ili 
uteuzi wao ukome mara moja. Maana hatuwezi kuacha akinamama wajawazito 
wapoteze damu wakati wa kujifungua, watu wanaopata ajali wapoteze maisha
 kwa sababu ya watu hawataki kutimiza wajibu wao.
Hilo
 haliwezi kukubalika, Mfumo wa hali ya damu kwa Tanzania kwa sasa 
unatisha. Kwa sasa nchi inakiwango cha chini mno, tokea wafadhili 
wajiondoe katika hili. Ni lazima tuwe makini sana maana leo mzima kesho 
umepata ajali, umepasuka mfupa wa kwenye paja damu nyingi zimemwagika 
unahitaji damu!!
Kwa
 upande wa watu wote wanaopata damu salama nchini, huduma hiyo 
wanazipata bure kwani damu hizo ni za Serikali, Hata hivyo mifuko na 
vitu vinavyotumika kuhifadhia damu hiyo vina gharama kubwa.
“Damu
 inatolewa bure na serikali. Mtambue kuwa, vifaa vya kutunzia damu hii 
ni gharama kubwa. Hivyo mifuko mashirika ya Bima, na mashirika mengine 
kuanzia leo kutazama namna ya kulipa gharama za vifaa vya utunziaji damu
 hizo. Damu ni bure, lakini mfuko ule wa kutunzia ile damu ni gharama 
kubwa sana na hata vifaa vya kupimia damu ile nayo ni gharama kubwa 
hivyo walipie kwa kila damu watakayochukua.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Meneja
 wa kanda ya Mashariki Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo 
jijini Dar es Salaam, Eveline Mgassa (mwenye miwani) akielezea utaratibu
 wa ukusanyaji wa damu unavyofanyika kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
 ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyefanya 
ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016 jijini Dar.
Naibu 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
 Kingwangalla (aliyeipa mgongo kamera) akisikiliza maelezo kutoka kwa 
Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo 
jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma ya namna wanavyopokea watu 
wanaofikia kuchangia damu kwa hiari na kuhifadhiwa kwenye benki hiyo 
yaTaifa ya Damu Salama, alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016 
katika ofisi hizo.
Naibu 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi 
Kingwangalla akitoa mkono wa pongezi kwa wananchi walioonyesha uzalendo 
kwa kufika katika ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Januari 4, 
2016 na kuchangia damu kwa hiari yao ambapo mmoja kati yao alisema hii 
ni mara yake ya nne na ni utararibu aliojiwekea.
Naibu 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi 
Kingwangalla akisalimiana na kumpongeza mmoja wa wananchi (jina lake 
halikuweza kupatikana) aliyefika kuchangia damu kwa hiari, Januari 4, 
2016 katika makao makuu ya ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
Naibu 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi 
Kingwangalla akiwa ndani ya maabara ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama 
alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi hizo, Januari 4, 2015 jijini
 Dar es Salaam.
Naibu 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi 
Kingwangalla akisaini vitabu vya wageni nje ya ofisi za Mpango wa Taifa 
wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Januari 4, 2016 wakati 
alipofanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo.
Naibu 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi 
Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ziara 
ya kushtukiza na kuzungikia vitengo mbalimbali katika ofisi za Mpango wa
 Taifa wa Damu Salama jijini Dar es Salaam.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment