Mwenyekiti
 wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wapenzi na 
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla 
fupi ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli kwa ushindi alioupata katika 
uchaguzi wa uliofanyika oktoba 25 mwaka 2015. 
 Mwenyekiti
 wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia)akizungumza na Katibu 
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana(katikati) pamoja na Waziri Mkuu Mhe.
 Mizengo Pinda wakati wa sherehe ndogo ya kushukuru wapiga kura walioipa
 CCM ushindi.
 Rais
 Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote waliompigia 
kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba ambapo 
aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote
waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba
ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba
ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
 Rais
 Mteule Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kwa  wananchi 
waliojitokeza kumpongeza nje ya Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.
Rais
 Mteule Dk. John Pombe Magufuli akionyesha cheti alichokabidhiwa na Tume
 ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kushinda kiti cha Urais kwenye 
uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015.
 Mama
 Samia Suluhu aliyekuwa Mgombea Mwenza akionyesha cheti chake cha 
Umakamu wa Rais kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja 
kumpongeza.
 Rais
 Mteule Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mke wake Janeth Magufuli 
mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mteule wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli.
 Katibu
 wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza kwenye hafla hiyo ya 
kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya Ofisi Ndogo CCM Lumumba.
 Rais
 Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa jiji la Dar es Salaam
 mara baada ya kumalizika hafla ya kuwasalimu na kuwashukuru kwa 
kumpigia kura zilizompa ushindi wa kiti cha Urais.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya ofisi ndogo CCM Lumumba.
 
 
 
 
 
 














 
 
0 comments:
Post a Comment