Rais Dk.Jakaya Kikiwete akizundua kampuni ya Soko la Bidhaa katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
Rais Dk.Jakaya Kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na Menejimenti na Bodi ya Kampuni ya Soko la
Bidhaa wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dk.Jakaya Kikwete akizungumza
wakati uzinduzi wa Kampuni ya Soko la Bidhaa iliyofanyika katikza
ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam Oktoba 30, 2015.
Waziri wa Fedha na Uchumi,Saada Mkuya akizungumza na wakati uzinduzi wa kampuni ya Soko la bidhaa jijini Dar es Salaam.
Sehemu wataalam mbalimbali wakiwa wamekekti katika uzinduzi wa Kampuni ya Soko la Bidhaa jijini Dar es Salaam.
Rais Dk.Jakaya Kikwete amesema kuanza kwa kampuni ya soko la
bidhaa kutasaidia wakulima kupata soko la uhakika na kukuza uchumi
pamoja na kupata bima katika kilimo.
Hayo ameyasema leo wakati uzinduzi wa Kampuni ya soko la bidhaa
jijini Dar es Salaam,Dk.Kikwete amesema wakulima wamekuwa wakilima
lakini masoko yao hayana uhakika na kilimo hakina tija.
Amesema kuwa mfumo utasaidia wakulima kupata bei ya uhakika wa
kuuza mazao yao na wanunuzi kufahamu bei ya soko la bidhaa
wanayoihitaji.
Dk.Kikwete ameitaka watu wanaofanya kazi kuwa waaminifu katika
kuweza kuwafanya wakulima wanufaike na soko hilo kwa kuwaletea maendeleo
ya kuendeleza na kuachana na kutafuta masoko ambayo mwisho wa siku
wanauza kwa hasara.
Aidha amesema soko la bidhaa litawaondolea wakulima ukopwaji
ambao umekuwa ukiwakatisha tamaa na kushindwa kuendeleza kilimo chenye
tija.
Amesema wakulima wamekuwa wakifanya kazi zao za kilimo wakiwa na
changamoto kubwa ya kukosa soko la uhakika na kufanya mazao kununuliwa
na watu wachache kwa bei ya chini.
Dk.Kikwete amesema wakulima wakiwa wana soko la uhakika
kutafanya waweze kuingia katika bima kutokana na kilimo kuonyesha mwanga
katika sekta hiyo.Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Soko la Bidhaa (TMX),Nasama Masinda
amesema kuwa soko hilo wataanzia mazao ya Ufuta,Korosho pamoja na mpunga
.
Amesema wamejipanga katika kuhakikisha wanaweka uwazi wa soko
katika bidhaa hizo kwa wanunuzi na wauzaji kuwa na bei inayoendana na
soko.
0 comments:
Post a Comment