Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama Mjini, James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha Chadema.
Akiongea
katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo hilo, Lembeli amesema kuwa
hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na
shughuli alizokuwa akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Alisema
kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama
mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia
radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa
ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.
Pia,
Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi
kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea
kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza
kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.
Kadhalika,
Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na
jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa
kuwa mshindi.
0 comments:
Post a Comment