Kwenye list ya Wabunge wa upinzani ambao waliwahi kugusa vichwa vya habari na kutikisa Vikao vya Bunge lililopita Tanzania, David Kafulila wa Chama cha NCCR- Mageuzi
yumo !! YES.. Na kilicholiongezea uzito jina lake ilikuwa ishu ya
ESCROW, ambayo ilipelekea baadhi ya Mawaziri kuachia nafasi zao pamoja
na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Lakini jina lake pia halipo kwenye list
ya Wabunge ambao tunatarajia kuwashuhudia kwenye Bunge jipya
litakaloanza baada ya Uchaguzi Mkuu kukamilika, sababu inayopelekea hilo
ni matokeo ya Uchaguzi Mkuu kuonesha hakupata Kura za kutosha ili
awakilishe watu wake wa Kigoma Kusini Bungeni.
Kinachoendelea kwa sasa ni hiki kuhusu Ubunge wake >>>”Mpaka sasahivi ni suala ambalo linafanyiwa kazi na Mwanasheria anayeitwa Mpare Mpoki… Jumatatu ya wiki ijayo Kesi tutaiingiza Mahakama Kuu Tabora.”- David Kafulila.
“Ni
kesi ambayo inatakiwa kuandaliwa kwa weredi mkubwa kuepusha mapungufu,
lakini ni kesi fupi kwa sababu tunachokitaka ni ifahamike kwamba
aliyetangazwa siye aliyeshinda.” >>> David Kafulila.
Hii ilikuwa wakati wa Kampeni Kigoma, David Kafulila akinadiwa na aliyekuwa Mgombea Urais kupitia CHADEMA na UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa.
Kuna ushahidi unatakiwa? >>> “Hatuhitaji
mlolongo wa mashahidi isipokuwa fomu za Matokeo… Nilishinda mimi kwa
kura 34,000… nawahakikishia Wananchi wa Kigoma Kusini kwamba Kura zao
haziwezi kupotea, Wataongozwa na Mbunge ambaye walimchagua.” >>> David Kafulila.
“Tume
tuliyonayo ya Uchaguzi haijawa huru na ndio inapelekea mapungufu
kujitokeza… Kuna kasoro nyingi za Uchaguzi, ni matokeo ya mfumo… Kuna
taarifa kwamba kulikuwa na maelekezo toka Ikulu kwamba mpinzani wangu
atangazwe mshindi kwa sababu niliambiwa niachane na ESCROW lakini
sikukubali” >>> David Kafulila.
0 comments:
Post a Comment