MWENYEKITI
 wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga 
Mrema amesema kuwa kushindwa kwake ubunge kulitokana na michezo mchafu 
uliochezwa na mshindi wa ubunge wa jimbo hilo, Mwenyekiti wa Taifa wa 
Chama cha NCCR-MAGEUZI, James Mbatia
Akizungumza
 na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mrema amesema kuwa 
 mshindi wa jimbo hilo amekuwa akionywa na msimamizi  wa uchaguzi 
kutokana na matumizi ya vipeperushi ambavyo yeye alijipigia kura ya 
ubunge katika jimbo la Vunjo.
Mrema
 amesema matokeo ya yaliyompa ushindi Mbatia hakusaini kutokana na 
kufanya  hujuma nyingi ikiwa ni pamoja na  kumsema  mgombea mwenzake.
Aidha
 amesema kuwa  katika kipeperushi chake Mbatia sehemu ya bendera ya TLP 
yenye alama ya jogoo ilionekana kifaranga baada ya  kuwa na jogoo mkubwa
 anayewika.
Mrema
 katika kukutana na waandishi pia alimpongeza Rais Mteule wa CCM, 
Dk.John Pombe Magufuli kwa kura za kishindo na kutaka kuwa yuko naye.
Amesema
 kumpigia kampeni Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli kulitokana na 
kazi nzuri ya kupeleka barabara katika jimbo lake akiwa Waziri wa 
Ujenzi.
Mrema
 katika mkutano wake leo aliambatana na viongozi wa juu wa chama hicho 
kueleza hujuma alizofanyiwa katika uchaguzi katika jimbo la Vunjo 
akimhutumu, James Mbatia ambaye ameibuka kidedea katika uchaguzi huo.
Mwenyekiti
 wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP),Agustino Lyatonga 
Mrema akizungumza leo na waandishi habari juu ya kufanyiwa rafu katika 
jimbo la vunjo na kusababisha kushindwa kulitwa kwa mara nyingine 
kushoto ni aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP ,Maxmillian Lyimo , na Kulia 
 Katibu Mkuu wa TLP,Nancy Mricaria.
Waandishi
 wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti  wa Taifa wa Chama cha Tanzania 
Labour Party (TLP), Agustino Lyatonga Mrema leo jijini Dar es Salaaam.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment