Ni July 10, 2016 ambapo Tanzania imepata ugeni kutoka kwa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ambae kupitia ujio wake 
 ameahidi kusaidia katika utekelezaji wa Miradi ya Maji Dar es Salaam na
 Pwani, pia kusaidia kuendeleza sekta za Habari na Mawasiliano, Viwanda 
vidogo vidogo na Vyakati, Kilimo, Afya na masuala ya Usalama nchini, 
Ikulu  Dar es Salaam.
Baada ya Waziri hiyo kutoa ahadi hizo 
sasa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia kwenye ukurasa 
wake wa instagram alisema….‘Imekuwa
 siku ndefu ila yenyemafanikio makubwa sana kwa Taifa langu na 
watanzania wote. Hongera sana Rais wetu, hongera pia Waziri Mkuu wa 
India’- RC Paul Makonda
‘Karibu
 tena Tanzania. Fursa zinazotafutwa na viongozi wetu naomba tuzitumie 
tusiishie kulalamika tu. Sasa kilimo cha mazao jamii ya kunde soko lipo 
tena la uhakika. kwa tani laki 1 tunaigiza dola Milioni 300, je kwa tani
 Milioni 7 si itakuwa dola bilioni kadhaa. Vijana tuchangamke India 
wanahitaji zaidi ya tani Milioni 7 ya mazao ya kunde,choroko na dengu- RC Paul Makonda
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment