
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla amezindua Kivuko cha Kiteputepu
kijiji cha Mbaka Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya baada wananchi hao kupata
shida ya kuvuka na kuhatarisha maisha kwa Kuvusha Watoto kwenda Shule
kwa Kuogelea, kukosa huduma za Jamiii hasa Mto unapojaa Maji
Tarehe 10 Juni Mhe Jenista Mhagama,Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa alifika kujionea changamoto hiyo na Ofisi
yake ilichangia shilingi Milioni 10 na mnamo Tarehe 16 Juni Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Halmashauri alipatikana Mkandarasi na
alimpa Wiki 2 amalize Kazi na akahaidi Tarehe 8 Julai Kuwa tayari na
ahadi hiyo ameitimiza.
Gharama
ya Ujenzi wa Kivuko ni Shilingi Milioni 58 na kufuatia Uzinduzi huo
Wakazi wapatao 700 wa Kitongoji cha Kibundungulu wameanza kukitumia
Kivuko hicho kwa kupita kwa Miguu na Pikipiki
Amewataka
kukitunza Kivuko hicho kwani Ujenzi wa Daraja la kudumu unahitaji Fedha
nyingi zaidi ya Bilioni 1.5 hivyo ni vema wakakitunza kivuko hicho
kwasasa kwani kwa kiasi kikubwa kitapunguza tatizo la kuvuka na kwenda
Vijiji vingine

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mbaka Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya katika hafra ya uzinduzi wa Kivuko cha Kiteputepu.

Muonekano wa kivuko hicho kwa juu.

Baadhi ya wacheza ngoma wa kijiji cha Mbaka Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wakitoa burudani.








0 comments:
Post a Comment