Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe (Kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari wakati mkutano wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA) juu ya utekelezaji wa agizo la kusitisha usajili bodi za
wadhamini, Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa
Sifuni Mchome.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RITA, Emmy Hudson (Kulia) akitoa taarifa
ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Harrison
Mwakyembe la kusitisha usajili wa bodi za wadhamini leo jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe.
Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni
Mchome.
Sehemu ya wajumbe wa bodi wakimsikiliza Waziri wa Katiba na
Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa
wakati wa uchguzi mkuu kumekuwa na utitiri wa vikundi ambavyo
havionekani kazi zake na mwisho wa siku vinaomba msamaha wa kodi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Mwakyembe amesema kutokana na utitiri wa vikundi hivyo aliagiza Wakala
wa Usajili ,Ufilisi na Udhamini (RITA), kusitisha usajili wa vikundi
hivyo na kufanya uchambuzi ni vikundi ambavyo viko hai na vina vigezo
kwa mujibu wa sheria.
Amesema kufanya usajili wa vikundi ambavyo kimsingi hafifanyi kazi
iliyokusudiwa mwisho wa siku kuna uwezekano wa kusajili vikundi ambavyo
ni hatarishi kwa taifa.
Aidha amesema kuwa kutokana na uchambuzi ambao umefanywa na
kubainika kuwepo kwa vikundi 180 ambavyo vinatakiwa kufutwa kutokana na
kushindwa kutimiza masharti ya bodi za udhamini.
Mwakyembe baada uchambuzi huo ameitaka RITA kuendelea na kazi
usajili bodi za wadhamini kwa kufuata taratibu zote na kuwa na taarifa
zao.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (RITA), Emmy Hudson amesekuwa katika
uchambuzi huo kuna changamoto ambazo zilijitokeza ikiwa baadhi bodi za
wadhamini kubadili ofisi pamoja na kubadili majina bila kufuata sharia.
Amesema kuwa bodi za wadhamini wengine wanamiliki mali bila kufuata sheria kwa mujibu sheria za RITA.
0 comments:
Post a Comment