Katika
kupambana na wimbi la kupunguza umaskini hapa nchini, kampuni ya
Mawasiliano ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa “Airtel FURSA
Tunakuwezesha” unaendelea kutoa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kwa
vijana wenye lengo la kuwawezesha na kuwainua vijana hapa nchini .
Mafunzo
hayo ya biashara ambayo yamekuwa yakiendeshwa hapa nchini katika mikoa
mbali mbali , wiki ijayo yatafanyika Dar Live Mbagala Kuu karibu na Big
Bon siku ya Jumanne tarehe 15 ili kuwawezesha vijana kuweza
kukabiliana na wimbi hili gumu la kuendesha biashara na kuweza kukidhi
mahitaji yao ya kila siku na kuweza kuinua uchumi wa nchi hii.
Akizungumzia
kuhusu mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakiendelea hapa nchini, Meneja
huduma kwa jamii wa Airtel , bi Hwa Bayumi, alisema “mafunzo haya
yanalengo la kuwasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 18- 24 ambao
wanakiu ya kujikwamua na umasikini. Vile vile “Airtel FURSA
Tunakuwezesha” Airtel inawawezesha vijana kwa kuwapatia elimu ya
biashara na nyenzo za kuimarisha biashara zao.
Hivyo
basi tunapenda kuwakaribisha vijana wote waishio jijini Dar Es Salaam
kuweza kuhudhuria mafunzo haya ambayo yatatolewa bure kabisa bila
gharama yoyote. Ili kijana aweze kushiriki anatakiwa kufika pale Dar
Live siku ya jumanne tarehe 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi
jioni.
Vile
vile ili kijana kushiriki au kufaidika na mpango wa Airtel Fursa
atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo
yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo.
Pia
wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe
airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na
aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia
yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com>
aliongeza, Bayumi.
0 comments:
Post a Comment