JESHI
 la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao
 wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. 
Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka 
ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 
329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.
Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.
Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.
Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani.

Kamanda
 wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na waandishi 
wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na watuhumiwa 40 
washikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa tuhuma za ukwepaji 
kulipa kodi pamoja na mtu mmoja ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi 
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES 
LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini.
Kamanda
 wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akionyesha picha ya 
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR
 S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye 
anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM 
ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa 
wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND 
FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. 
Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa 
habari jijini Dar es Salaam leo.
Meneja
 wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania,
 Diana Masalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 
leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kukusanya jumla ya 
shilingi 10,075,979,462.08 kutoka kwa makampuni 22 ambayo yalihusika na 
uondoshwaji wa makontena bandarini kinyume cha sheria na taratibu za 
forodha hadi kufikia tarehe 10 Desemba 2015. 
Pia
 kati ya hao makampuni 06 amesema kuwa yamelipa kodi yote iliyokadiriwa 
pamoja na adhabu, ambapo makampuni 16 yamelipa sehemu ya kodi 
iliyokadiriwa pamoja na adhabu. 
Aidha, makampuni 26 hayajalipa kodi kiasi cha shilingi 4,789,924,609.69 pamoja na kwamba zoezi la ukadiriaji limefanyika. 
hata
 hivyo amesema kuwa leo ni siku ya mwisho iliyotolewa na Mheshimiwa Rais
 kwa wafanyabiashara waliokwepakulipa kodi ya makontena,
Amewasisitiza
 wananchi wote watoe taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia 
namba 0784210209. Pia taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio 
waadilifu zitolewe kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689 
122516.
 
0 comments:
Post a Comment