Jana Rais wa Tanzania John Magufuli alitangaza Baraza jipya la Mawaziri, likiwa na jumla ya Wizara 18 pamoja na Mawaziri 19.
Wadau wengi nchini wametoa maoni yao kuhusu uteuzi huo wakiwemo Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM.
Katika maoni yao UVCCM kupitia kwa Katibu wa Idara ya Uhamasishaji Egla Obed wamempongeza
 Rais kwa uteuzi mahiri na makini wa Baraza hilo ambalo ni dogo lakini 
limekamilika katika kuhakikisha linagusa kila sekta na kuhakikisha 
linapunguza na kubana matumizi yasiyo ya lazima.
Kuhusu uteuzi wa Mawaziri wengi vijana, UVCCM amesema haya >>> “Tumeridhishwa
 na uteuzi huu ambao umesheheni mawaziri na Manaibu wenye uwezo na 
weledi mkubwa sana, hatuna mashaka kwamba watafanya kazi kwa kasi na 
uzalendo, tumefarijika zaidi kwa kuwa lina vijana wengi ambao ni nguvu 
kazi ya Taifa, tunaiona dhamira ya dhati ya Rais kuhakikisha Tanzania 
inapata mabadiliko ya haraka” >>> Egla Obed.
Na kuhusu  ishu kazi na kasi ya Rais Magufuli je? Majibu yao ni haya >>> “Serikali
 itimize wajibu wake wa kuhakikisha inawawezesha wananchi kiuchumi na 
Mawaziri wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanaendeleza mapambano ya kubana
 matumizi yasiyo ya lazima ili fedha zielekezwe kwenye kuboresha huduma 
za kijamii, Watanzania hatatuwaelewa Mawaziri wetu kama hawatofuata 
maagizo ya Chama yaliyoanza kutekelezwa kwa kasi na Rais” >>> Egla Obed.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment