Baraza la Madiwani katika halmashauri ya
 Jiji la Mwanza leo limeketi katika kikao chake cha kwanza ambapo 
kimetoa fursa kwa Madiwani wateule kuapishwa na kuwachagua Meya na Naibu
 Meya wa Jiji la Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Baada ya Madiwani hao kuapa chini ya 
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mkoa wa Mwanza, Yusto Rubogoroga, walimchagua 
James Marwa Bwire ambae ni diwani wa Kata ya Mahina CCM (kulia) kuwa 
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na Naibu Meya akachaguliwa diwani wa 
Kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha (Kushoto) CCM.
Kwa nafasi ya Mstahiki Meya, James Marwa
 Bwire alipata kura 20 dhidi ya aliekuwa mgombea wa Chadema akiwakilisha
 pia Ukawa John Justine Pambalu ambae ni diwani wa Kata ya Butimba 
(Chadema) aliepata kura Tano huku Bhiku Kotecha akipata pia kura 20 
dhidi ya kura Tano alizopata mgombea wa Chadema akiwakilisha Ukawa 
Samwel Range Mwirabi ambae ni diwani wa Kata ya Pamba (Chadema). Jumla 
ya wapiga kura walikuwa 25. Hakuna kura zilizoharibika.
Diwani wa Kata ya Mahina (CCM) James Marwa Bwire akiapa kiapo cha kuwatumikia wananchi wa Kata hiyo.
Diwani wa Kata ya Butimba (Chadema) John Justine Pambalu akila kiapo cha kuwatumikia wananchi
Diwani wa Kata ya Pamba (Chadema) Samwel Range Mwirabi akila kiapo
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) 
Stanslaus Mabula akiapa kuwatumikia wananchi. Mbunge wa jimbo pia ana 
nafasi ya kuingia katika baraza la Madiwani katika halmashauri yake.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) 
Stanslaus Mabula akiapa kuwatumikia wananchi. Mbunge wa jimbo pia ana 
nafasi ya kuingia katika baraza la Madiwani katika halmashauri yake.
Madiwani Jijini Mwanza wakiapa kuwatumikia wananchi
Madiwani Jijini Mwanza wakiapa kuwatumikia wananchi
Diwani wa Kata ya Butimba (Chadema) John Justine Pambalu 
Madiwani halmashauri ya Jiji la Mwanza
Wanahabari
Wananchi na viongozi mbalimbali wakifuatilia kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani Jijini Mwanza.
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment