Rais mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli akionesha cheti chake cha 
ushindi alichokabidhiwa muda huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee
Na Anitha Jonas na Beatrice Lyimo- MAELEZO.
Watanzania wametakiwa
kukubaliana na matokeo ya  Uchaguzi
Mkuu  wa mwaka 2015, yaliyotangazwa na
Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kwa kuwa  ni ya haki na hakuna aliyeibiwa kura.
Hayo yamesemwa na
Mwenyekiti wa Waangalizi wa Uchaguzi kutoka nchi za Jumuiya ya Madola nchini na
ambaye Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodlucky Jonathan kwenye halfa ya kumkabidhi
hati Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka
Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika  leo
kwenye ukumbi wa Diamond  Jubilee  jijini Dar es salaam.
“Uchaguzi ulikuwa wa
haki na amani na hakuna yeyote aliyeibiwa haki yake kwani matokeo hayo yamedhibitishwa
kuwa ya uhuru na haki kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu zilizopo”
alisema  Rais Mstaafu Jonathan.
Kwa upande wa mgombea
urais kupitia chama cha ACT wazalendo Bibi. Anna Mghwira amesema kuwa chama
chake kimemkubali matokeo ya uchaguzi uliompitisha Dkt. John Magufuli.
Vilevile ameongeza kuwa
wagombea wote walizungumza kuhusu mabadiliko hivyo ana imani na mshindi wa
nafasi hii atalisimamia ipasavyo.
“Watanzania wanahitaji
mabadiliko hasa katika Katiba Mpya itakayotokana na maoni ya Watanzania, kuimarisha
umoja wa kimataifa, kuinua uchumi wa nchi, kusimamia shughuli za Serikali
pamoja na kuboresha usawa wa kijinsia kati ya mwanamke na mwanamume,” aliongeza
Bibi Mghwira.
Mbali na hayo mgombea
huyo wa urais kupitia chama cha ACT wazalendo amemkabidhi Rais Mteule Ilani ya
chama hicho kama muongozo kwa yale yaliyopungua katika Ilani ya cha chake.
Aidha Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewapongeza wananchi
kwa kuwa na mwamko mkubwa wa kupiga kura na kuliendesha zoezi hilo kwa amani.
Pia Jaji Mstaafu Lubuva
alimkabidhi hati ya ushindi mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika
uchaguzi.
 
 
 
 
 
 

 
 
0 comments:
Post a Comment