Bado tupo kwenye headlines za uchaguzi 2015 ambapo msanii mkongwe wa HipHop Tanzania Joseph Haule (Profesa Jay) ni mmoja wa wawashindi wa kiti cha ubunge kwenye uchaguzi huu akiwa amechukua jimbo la Mikumi Morogoro na anachosubiri kwa sasa ni kuingia bungeni.
Prof. ameongea na millardayo.com >>>‘Nawashukuru
sana wananchi wa Mikumi kwa kuniamini na kunipa dhamana hii kubwa,
watanzania wameniamini kwa sababu ya upeo mkubwa ambao Mungu
amenipa, naamini sana katika umoja na mshikamano….! na ndiomaana
nimekuwa nasisitiza hata katika kampeni zangu, lazima tushikamane watu
wote wa vyama vyote na hata wasio na vyama ili kuikomboa Mikumi yetu ‘ –
‘Changamoto
kubwa ni maji, elimu, miundo mbinu pamoja na ajira, nitaendelea
kuwatumikia wananchi wangu kwasababu wao ndio wamenituma Dodoma, mimi
kuwa mwanamuziki halitonizuia kuwawakilisha wananchi…. nitaendelea kuwa
mwanamuziki na huwenda nikafanya muziki ule wa juu zaidi kwasababu
nategemea kukutana na watu wa juu zaidi’– PROFESSOR J
Unaweza ukabonyeza play hapa chini kumsikiliza Professor Jay akizungumza kuhusu ushindi wake wa kiti cha Ubunge
0 comments:
Post a Comment