Kama bado hujaamua ni wapi unahitaji 
kuhifadhi pesa zako, au una account yako kwenye Benki ambayo 
hujaridhishwa na huduma zake, basi una kila sababu kusogelea moja ya Matawi ya Benki ya DTB na iwe ndio mkombozi wako kuanzia sasa.
Ninayo taarifa kutoka Benki hiyo na 
nimeona uko umuhimu wa kuifikisha kwako pia mtu wa nguvu, kwanza ni 
kwamba DTB inakuhakikishia huduma mahali popote kwa sababu inafungua 
Matawi mapya manne kila mwaka ndani ya Tanzania >>> “Mambo
 mawili muhimu ni kuhusu uuzaji wa Hisa kwa wamiliki wa Benki, ambapo 
tumefanikiwa kukusanya Bilioni 30 kutokana na mauzo ya hisa hizo… hii 
imeimarisha mtaji wa Benki, kuwekeza kwenye Matawi mapya, teknolojia na 
uanzishaji wa huduma mpya“– Hii ni nukuu ya kilichosemwa na Joseph Mabusi, ambaye ni Chief Finance Officer wa Benki ya DTB.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DTB Tanzania, Viju Cherian.
Uthibitisho mwingine ni huu kwamba kila Benki ya DTB inajali kumhudumia kila mtu >>> “Mwaka
 2015 tumeweza kuanzisha account za watoto, akina mama, wazee na account
 maalum kwa ajili ya wanafunzi ambayo tunaiita ‘KISOMI ZAIDI’… Hii 
inatokana na ukuaji wa Benki kila mwaka” — Joseph Mabusi.
Mengine ya kukufikia ni haya mtu wangu >>> “DTB
 ina jumla ya miaka 70 tangu imeanzishwa, una kila sababu ya kuiamini… 
mpaka mwezi wa Septemba 2015, DTB imepata faida ya BILIONI 20, ni 
ongezeko la zaidi ya 30% ukilinganisha na faida ya mwaka 2014” >>> Joseph Mabusi.
Matawi ya Benki je? >>> “Benki
 ina matawi 24 Tanzania, kati ya hayo Matawi 10 yako Dar es Salaam… 
mengine yako Arusha, Mbeya, Mwanza, Kahama, Tabora, Zanzibar, Tanga, 
Dodoma, Iringa, Mtwara, Moshi na Morogoro… “- Joseph Mabusi
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment