Taarifa ninayokusogezea ni ya David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, tunafahamu ana kesi Mahakamani ya kupinga matokeo ya ubunge 2015 jimbo
la Kigoma Kusini kesi ipo Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, taarifa
ikufikie kuwa Kafulila baada ya kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma
akasomewa kesi mpya ambayo anakiri hakuwa anaifahamu mwanzo kwenye
sentensi zake; – David Kafulila
David Kafulila
‘Nilifikishwa mahakamani kwa kesi mpya ukiachilia kesi ya kwanza ya kupinga matokeo ya uchaguzi 2015
jimbo la Kigoma kusini, awali nilikuwa nikijua ninakesi moja katika
mahakama ya hakimu mkazi kigoma kwa madai kwamba nilimdhalilisha
aliyekuwa mkuu wa wilaya Khadija Nyembo tangu mwaka 2013….nikiwa mahakamani nikapewa tena kesi nyingine ni kesi ya kuhamasisha wananchi wasichangie mchango wa maabara; – David Kafulila
‘Bado
msimamo wagu utabaki palepale kwamba nitaendelea kupigania nchi yangu,
kesi hizi zote katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma ukitazama hati za
mashitaka yote ya Kafulila hapa Kigoma zimeandaliwa na kusainia na DPP makao makuu Dar es salam inawezekanaje;- Kafulila
0 comments:
Post a Comment