BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016
BODI
  ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuutaarifu umma kuwa 
kuna taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi 
haitatoa mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016. 
Taarifa hizo si za kweli na hivyo Bodi inauomba umma kuzipuuza. 
Aidha,
 Bodi ya Mikopo inapenda kutoa taarifa kwamba hadi sasa 
imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 40,836 wa 
mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla 
ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo na katika Awamu ya Pili 
iliyotolewa tarehe 9 Novemba, 2015 jumla ya waombaji 28,554 wamepangiwa 
mikopo.
Majina
 ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili 
yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya 
Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa 
ajili ya taratibu za usajili.
Lengo
 la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa 
kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016, ambao ni 50,830, 
wanapata mikopo.
Aidha,
 Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato
 wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa unaendelea.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
 
 
 
 
 
 


 
 
0 comments:
Post a Comment