Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Donan Mmbando akizungumza na
waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Mlipuko wa Ugonjwa wa
kipindupindu uliopo sasa ulianza mnamo 15 Agosti 2015, katika Manispaa
ya Kinondoni na baadae kusambaa katika Manispaa zote za Mkoa wa Dar es
Salaam leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Donan Mmbando, leo jijini Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MLIPUKO wa Ugonjwa wa kipindupindu umesambaa katika mikoa 14 na kufikia wagonjwa 7825 na vifo 106.
Akizungumza
na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii, Donan Mmbando amesema kati ya wagonjwa wote
waliougua 3746 sawa na asilimia 67 wanatoka katika mkoa wa Dar es
Salaam.
Amesema
kuwa Mikoa inayotoa taarifa ya kuwepo wagonjwa wapya ni Dar es Salaam,
Morogoro, Pwani, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mara, Singida na Tanga.
Mmbando
amesema kuwa ugonjwa huo umeripotiwa katika mikoa mingine ya Tanzania
ikiwa ni pamoja na Pwani, Singida, Mara, Arusha, Tanga, Mwanza,
Shinyanga, Morogoro, Iringa, Kilimanjaro, Dodoma, Kigoma, Geita pamoja
na Rukwa.
Aidha
amesema hadi kufikia Novemba 8,2015 idadi ya wagonjwa waliokwisha
kuripotiwa tangu mlipuko uanze hapa nchini ni 7825 na vifo 106 amabo ni
asilimia 1.3 ya waliougua.
Amesema
hatua walizozichukua kwa ugonjwa huo ni kutoa dawa, vifaa vya maabara
na vifaa kinga kwa mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro.
Aliongeza
kuwa Wizara imepokea maombi kutoka mikoa ya Singida, Arusha, Tanga,
Mwanza, Mara na Geita kati ya Oktoba 15 mwaka huu na yanashughukuliwa
na utawala, Kupima vipimo vya maabara na kufuatilia ubora wa vipimo
kutoka katika mikoa iliyofanya uchunguzi na kuthibitisha uwepo wa
ugonjwa huo, Kupeleka timu za watalaam kutoka ngazi ya Mkoa na Taifa
kusaidiana na timu za Wilaya husika.
Aidha
tarehe 28 Oktoba 2015, Timu ya Kitaifa ilienda katika mikoa ya Tanga, na
Singida na vilevile mkoa wa Manyara pia timu ilienda kwa ajili ya
kufuatilia tarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa kuhara na kutapika – taarifa
ya timu hizi inakamilishwa na itawasilishwa.
Mmbando
amesema hatua nyingine Kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya juu ya
ufuatiliaji wa ugonjwa na utoaji wa matibabu ,Kutoa elimu ya kwa umma
kupitia vyombo vya habari hususani radio na runinga. Aidha, mafunzo kwa
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini
yametolewa, Kuandaa “Water safety plan” kwa kushirikisha wadau
mbalimbali ikiwemo WHO, PSI, CDC, MSF, Redcross na USAID. Aidha mpango
mkatati huu utajikita kwanza kwa jiji la Dar es salaam kwa kuanzia na
hapo baadae itaenda katika mikoa mingine.
Amesema
changamoto katika ugonjwa huo ni,Mwitikio hafifu wa jamii juu ya
kukabiliana na ugonjwa huu,Jamii kutokuzingatia kanuni za afya na
mazingira,Ushiriki mdogo wa sekta nyingine katika kupambana na ugonjwa
huu,Ukosefu wa pesa za kuwalipa watumishi wa afya wanaohusika katika
zoezi la kukabiliana na ugonjwa huu.
0 comments:
Post a Comment