Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama
Samia Suluhu Hassan, akipokea nyaraka za Ofisi kutoka kwa Makamu wa Rais
Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa makabidhiano ya Ofisi
yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo No 9, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisaini Kitabu cha wageni wakati
alipoingia Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa Ofisi na
Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Nov 9, 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama
Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa
Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia kwake), Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Makamu wa Rais, Sazi Salula na Naibu Katibu Mkuu wake, baada ya
makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Nov 9,2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya
Makamu wa Rais, baada ya bakabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika Ikulu jijini Dar
es Salaam, leo Nov 9, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa
Ofisi yake wakati alipowasili kwenye Ofisi yake kwa mara ya kwanza leo baada ya
kukabidhiwa rasmi Ofisi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Bilal. Wafanyakazi hao
walijipanga kumpokea huku wakiimba, kupiga makofi na vigeregre wakati
akiwasili.
0 comments:
Post a Comment