Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jami.
CHAMA
cha wafanyakazi wa viwanda na sekta mbalimbali(IGWUTA) champongeza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli
(Pichani)kwa namna na jinsi anavyofanya kazi yake hasa ile ya kupambana
na mafisadi na wanafiki.
Akizungumza
na Waandishi wa habari leo Katibu Mkuu wa chama chama cha IGWUTA,
Michael Kashamba amesema kuwa,Wamefurahishwa kwa kumpata Rais Magufuli
na wanatoa wito kwa Wafanyakazi wote hapa nchini kujitokeza na kumuunga
mkono Rais wetu katika mapambano dhidi ya ufisadi.
Aidha
Kashamba ametoa tamko la kumpongeza Magufuli kuwa ni kiongozi asiyekuwa
wa kawaida, Hana ubinafsi na anaweka maslahi ya nchi mbele huku
akimfananisha kwa utendaji wa kazi zake ni kama Rais wa awamu ya kwanza
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Pia Kashamba
amesema kuwa, Chama chao kinatoa huduma ya kuelimisha na kuhamasisha
wanachama kutimiza wajibu wao wa kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na
uaminifu mkubwa.
Pia IGWUTA inatoa Huduma za utetezi kwa Wanachama dhidi ya uonevu wowote uliofanywa na baadhi ya waajiri hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment