Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akiwasili Makao Makuu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), Kinondoni jijini Dar es Salaam na kupokewa na Mkurugenzi
Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu (kushoto). Waziri Kitwanga alifanya ziara ya
kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali
zinazofanywa na mamlaka hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Afisa Usajili wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Brenda Joshua akimfafanulia Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai), jinsi
wanavyosajili taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho. Waziri
Kitwanga alitembelea Kituo hicho cha Usajili na kujifunza kazi
mbalimbali zinazofanywa na NIDA, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu
Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na kulia kwa Abdulwakil ni Naibu
Katibu Mkuu, John Mngodo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (katikati) akiieleza jambo menejimenti ya Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao
Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil,
wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo, na
watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment