Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu akitoa taarifa mbalimbali za shughuli zinazofanywa na
jeshi hilo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
(katikati), wakati Waziri huyo alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi
hilo, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza na Viongozi Wakuu wa
jeshi hilo, ambapo walikubaliana kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na
uhalifu nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
mara baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi
nchini. Waziri Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari kuwa,
wamekubaliana na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo kuweka mikakati zaidi ya
kukabiliana na uhalifu nchini. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
Wapili kulia meza kuu ni Naibu IGP,
Abdulharam Kaniki. Kulia ni Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi
hilo, Paul Chagonja. Kushoto meza kuu ni Kamishna wa Polisi Jamii
nchini, Mussa Ali Mussa. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya
Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (katikati waliokaa), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,
IGP Ernest Mangu (watatu kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja
na Viongozi wa Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kikao chao
kilichofanya katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo
kumalizika. Waziri Kitwanga alifanya mazungumzo na Viongozi hao na
kukubaliana kuweka mikakati ya kupambana na uhalifu.
Msafara wa Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ukiwasili katika lango Kuu la Makao
Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya
mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi hilo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Ernest Mangu wakati alipokuwa anawasili Makao Makuu ya Jeshi
hilo, jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi. Waziri Kitwanga
alifanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo na kukubaliana
kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment