Pages

Ads 468x60px

Wednesday, October 26, 2016

FULL TIME EFL CUP: MANCHESTER UNITED 1 v 0 MANCHESTER CITY, MATA AMBEBA MORINHO NYUMBANI OLD TRAFFORD!


English Football League Cup, Football League Cup - Fourth Round

VIKOSI:
Man Utd wanaoana XI:
De Gea, Valencia, Rojo, Blind, Shaw, Carrick, Ander Herrera, Mata, Pogba, Rashford, Ibrahimovic
Akiba: Depay, Lingard, Young, Romero, Fellaini, Schneiderlin, Darmian
Man City: Caballero, Maffeo, Otamendi, Kompany, Clichy, Garcia, Fernando, Sane, Jesus Navas, Iheanacho, Nolito
Akiba: Sterling, Gundogan, Aguero, Kolarov, Fernandinho, Adarabioyo, Gunn

Sunday, July 10, 2016

MATUMIZI YA TIKETI ZA KAWAIDA KATIKA MABASI YA UDART MWISHO JULAI 30 MWAKA HUU



Mabasi ya Shirika la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART) yakiwa makao makuu ya Udart Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), David Mgwassa (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu matumizi ya kadi badala ya tiketi. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari.
Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja wa Uhusiano wa Udart, Deus Bugaywa (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea

Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (UDART), imetangaza kaunzia Julai 30 mwaka huu kuwa ni mwisho wa matumizi ya tiketi za kawaida kwa abiria badala yake zitatumika kadi.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwassa wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu matumizi ya kadi badala ya tiketi.

" Tiketi zitaendelea kutumiwa na wanafunzi lakini watu wengine wote watatumia kadi maalumu za kupandia mabasi yetu" alisema Mgwassa.

Alisema Udart imepunguza bei ya kadi hizo kutoka sh.4500 ya awali hadi kufikia sh.2000 ili kutoa fursa kwa kila mwananchi wa kuweza kuipata kadi hizo na kuzitumia.

Mgwassa alisema kadi ziliuzwa ni 55,000 na zilizobaki ni 150,000.

Mkuu wa idara ya Fedha wa Kampuni ya MaxMalipo walioingia ubia ma Udart katika mpango huo, Deogratius Lazari alisema wateja wataweza kulipia kadi hizo kupitia kwa mawakala wao waliopo katika vituo vyote vya udart na kwa njia ya mitandao yote ya simu.

India yaipatia Tanzania dola milioni 500 za Kimarekani kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo



India imeipatia Tanzania dola za Kimarekani milioni 500 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ili kukuza ushirikiano wa kiuchumi baina nchi hizi mbili
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika dhifa ya kitaifa aliyomwandalia mgeni wake, Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi.
“Tunaishukuru India ambayo imeonyesha utayari wa kushirikiana nasi kiuchumi katika kilimo, TEHAMA, maji, Elimu, Afya na Ulinzi,” amesema Rais Magufuli.Rais Magufuli pia amesema ushirikiano wetu na India utatoa fursa kwa Tanzania kutimiza azma yake ya kuwa na uchumi wa viwanda kwani katika ziara hii Waziri Mkuu ameambatana na wafanyabiashara takriban 50 ambao wanaangalia fursa za kibiashara hapa nchini.

“India ni mdau wetu mkubwa wa  kibiashara  na uhusiano huu umekuwa ukikua kwani mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini India yameongezaka toka thamani ya  dola za kimarekani milioni 187 mwaka 2005 hadi dola bilioni 1.29 mwaka 2015,”alisema Rais Magufuli.Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa India itatoa fedha kwa nchi ya Tanzania kwa ajili ya kilimo cha Dengu ambayo ni fursa ya ajira kwa watanzania na kuinua kipato cha wananchi.

Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake na miradi ya India ikiwemo mradi unaojulikana kama Making India, mradi ambao unatumia malighafi zinazopatikana nchini na kutumia nguvu kazi ya nchini ambao utapunguza tatizo  la ajira katika Taifa la Tanzania.

Amebainisha kuwa India iko tayari kushirikiana na Tanzania kwenye miradi ya gesi ikizingatiwa kuwa aina mbali mbali za gesi zinazidi kugunduliwa hapa nchini. Katika suala la gesi India iko tayari kutoa utaalamu na wataalamu kwa ajili miradi ya gesi.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa India , Mhe. Narendra Modi ameishukuru Tanzania kwa ukarimu alioupata hapa nchini na akaahidi kuendeleza ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili.Amesema India italeta watu wake, utaalaamu na teknolojia yake kwa Tanzania, jambo ambalo litaongeza ushirikiano wa kiuchuni kati India na Tanzania.

Waziri Mkuu huyo amemaliza ziara yake ya kiserikali  ya siku mbili nchini na kuondoka kuendelea na ziara katika nchi nyingine za Ukanda wa Afrika Mashariki.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi aondoka nchini baada ya kukamilisha ziara ya siku mbili nchini Tanzania




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akishukuru kabla ya kuondoka baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akipungia mkono vikundi vya utamaduni vilivyokuwa vikitoa buradani katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiwa na watoto wa Kitanzania wenye asili ya kihindi kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi akiwa na watoto wa Kitanzania wenye asili ya kihindi kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wafanyakazi wa kitengo cha mizigo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JINIA jijini Dar es Salaam mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. PICHA NA IKULU


India na Tanzania zasaini mikataba ya miradi ya maendeleo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.




Na. Immaculate Makilika- MAELEZO


Serikali ya India na Tanzania zimesaini mikataba ya miradi ya maendeleo katika sekta za maji, kilimo, viwanda, teknolojia ya habari na mawasiliano na afya katika kuimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili ili kusaidia wananchi wake.


Mikataba hiyo imesainiwa leo, wakati Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi alipokua akifanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.


Mikataba wa kwanza uliosainiwa inahusisha mradi wa kusambaza maji katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.


Aidha, mkataba wa pili unahusisha mradi wa kusambaza maji Zanzibar ambao unatarajiwa kugharimu dola  za kimarekani milioni 92 ambapo mradi huo unatarajiwa kufikia miji 17 nchini na mkataba mwingine utahusisha mafunzo ya ufundi yatakayosaidia kuzalisha wataalamu mbalimbali.


“Lengo letu ni kusaidiana  na kuimarisha mahusianao yetu katika kukuza uchumi na kutengeneza fursa mpya za ajira kwa wananchi wetu” alisema Waziri Modi.


Waziri Modi aliongeza kuwa Serikali ya India itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa biashara na hatimaye kukuza uchumi wa nchi hizo.


Kwa upande wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alisema Serikali India imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania hasa katika masuala ya maendeleo ambapo imeweza kuwekeza nchini kiasi shilingi za Kimarekani dola bilioni 2.4 na kuzalisha  ajira 54,176.


Baadhi ya misaada iliyotolewa na Serikali ya India ni pamoja na  mashine ya vipimo vya ugonjwa wa kansa katika hospitali ya Bugando, itakayosaidia wakazi wa kanda ya ziwa na nchi nzima kwa ujumla pamoja na kuongeza na kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika la viwanda vidogo vigodo la India kushirikiana na Tanzania katika kukuza viwanda vidogo na vya kati nchini.


Katika masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano, Serikali hiyo imeahidi kuleta wataalamu wao nchini Tanzania kwa lengo la kutengeneza program mbalimbali ili kuisaidia Tanzania katika masuala ya ulinzi wa mitandao pamoja na kutengeneza namna bora za ukusanyaji wa mapato ya nchi.


Katika masuala ya viwanda, Serikali ya India imeahidi kuanzisha viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu  zitakazotibu   magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria, figo na kisukari, ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa tiba vitakavyotumika katika hospitali mbalimbali nchini kwa lengo la kupunguza gharama ya kununua vifaa hivyo nje ya nchi.


Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa nchi ya India ina uhitaji mkubwa wa mazao ya kilimo hasa jamii ya kunde hivyo akawataka wakulima kutumia fursa hiyo kuzalisha mazao hayo kwa wingi.


“India inauhitaji wa tani 200 za mazao jamii ya kunde, wakulima mnatakiwa kuzalisha mazao hayo kwa wingi kwa vile tayari kuna soko la uhakika, na tutahakikisha madalali hawatakuwepo ili mkulima asikandamizwe” alisema Rais Magufuli.


Katika sekta ya uwekezaji nchini, India ni nchi ya tatu kwa uwekezaji Tanzania ikifuatiwa na Uingereza pamoja na China.

Sentensi za RC Paul Makonda kuhusu ugeni wa Waziri Mkuu wa India…


Ni July 10, 2016 ambapo Tanzania imepata ugeni kutoka kwa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ambae kupitia ujio wake  ameahidi kusaidia katika utekelezaji wa Miradi ya Maji Dar es Salaam na Pwani, pia kusaidia kuendeleza sekta za Habari na Mawasiliano, Viwanda vidogo vidogo na Vyakati, Kilimo, Afya na masuala ya Usalama nchini, Ikulu  Dar es Salaam.
Baada ya Waziri hiyo kutoa ahadi hizo sasa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alisema….‘Imekuwa siku ndefu ila yenyemafanikio makubwa sana kwa Taifa langu na watanzania wote. Hongera sana Rais wetu, hongera pia Waziri Mkuu wa India’- RC Paul Makonda
Karibu tena Tanzania. Fursa zinazotafutwa na viongozi wetu naomba tuzitumie tusiishie kulalamika tu. Sasa kilimo cha mazao jamii ya kunde soko lipo tena la uhakika. kwa tani laki 1 tunaigiza dola Milioni 300, je kwa tani Milioni 7 si itakuwa dola bilioni kadhaa. Vijana tuchangamke India wanahitaji zaidi ya tani Milioni 7 ya mazao ya kunde,choroko na dengu- RC Paul Makonda

Friday, July 8, 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA AZINDUA KIVUKO CHA KITEPUTEPU WILAYANI RUNGWE NA KUWATAKA WANANCHI KUKITUNZA KITEPUTEPU HICHO..


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Mh.Amos Makalla amezindua Kivuko cha Kiteputepu kijiji cha Mbaka Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya baada wananchi hao kupata shida ya kuvuka na kuhatarisha maisha kwa Kuvusha Watoto kwenda Shule kwa Kuogelea, kukosa huduma za Jamiii hasa Mto unapojaa Maji 

Tarehe 10 Juni Mhe Jenista Mhagama,Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa alifika kujionea changamoto hiyo na Ofisi yake ilichangia shilingi Milioni 10 na mnamo Tarehe 16 Juni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Halmashauri alipatikana Mkandarasi na alimpa Wiki 2 amalize Kazi na akahaidi Tarehe 8 Julai Kuwa tayari  na ahadi hiyo ameitimiza.

Gharama ya Ujenzi wa Kivuko ni Shilingi Milioni 58 na kufuatia Uzinduzi huo Wakazi wapatao 700 wa Kitongoji cha Kibundungulu wameanza kukitumia Kivuko hicho kwa kupita kwa Miguu na Pikipiki

Amewataka kukitunza Kivuko hicho kwani Ujenzi wa Daraja la kudumu unahitaji Fedha nyingi zaidi ya Bilioni 1.5 hivyo ni vema wakakitunza kivuko hicho kwasasa kwani kwa kiasi kikubwa kitapunguza tatizo la kuvuka na kwenda Vijiji vingine

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mbaka Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya katika hafra ya uzinduzi wa Kivuko cha Kiteputepu.
Muonekano wa kivuko hicho kwa juu.
Baadhi ya wacheza ngoma wa kijiji cha Mbaka Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wakitoa burudani.


DOLE LA KATI LA MBUNGE MR SUGU LILILOSABABISHA AFUNGIWE BUNGENI



Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Mr Sugu' akiwaonesha wabunge wa CCM dole la kati Bungeni Dodoma hivi karibuni, kitendo ambacho kilitafsiliwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa ni tusi, hivyo kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao kumi vya Bunge.

NEWZ ALERT:Rais Magufuli amteua Dkt. Leonard Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS



UTITIRI WA VIKUNDI HUIBUKA KATIKA KIPINDI CHA UCHAGUZI-DK.MWAKYEMBE.



Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati mkutano wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) juu ya utekelezaji wa agizo la kusitisha usajili bodi za wadhamini, Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RITA, Emmy Hudson (Kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Harrison Mwakyembe la kusitisha usajili wa bodi za wadhamini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
Sehemu ya wajumbe wa bodi wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa wakati wa uchguzi mkuu kumekuwa na utitiri wa vikundi ambavyo havionekani kazi zake na mwisho wa siku vinaomba msamaha wa kodi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwakyembe amesema kutokana na utitiri wa vikundi hivyo aliagiza Wakala wa Usajili ,Ufilisi na Udhamini (RITA), kusitisha usajili wa vikundi hivyo na kufanya uchambuzi ni vikundi ambavyo viko hai na vina vigezo kwa mujibu wa sheria.
Amesema kufanya usajili wa vikundi ambavyo kimsingi hafifanyi kazi iliyokusudiwa mwisho wa siku kuna uwezekano wa kusajili vikundi ambavyo ni hatarishi kwa taifa.
Aidha amesema kuwa kutokana na uchambuzi ambao umefanywa na kubainika kuwepo kwa vikundi 180 ambavyo vinatakiwa kufutwa kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya bodi za udhamini.
Mwakyembe baada uchambuzi huo ameitaka RITA kuendelea na kazi usajili bodi za wadhamini kwa kufuata taratibu zote na kuwa na taarifa zao.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (RITA), Emmy Hudson amesekuwa katika uchambuzi huo kuna changamoto ambazo zilijitokeza ikiwa baadhi bodi za wadhamini kubadili ofisi pamoja na kubadili majina bila kufuata sharia.
Amesema kuwa bodi za wadhamini wengine wanamiliki mali bila kufuata sheria kwa mujibu sheria za RITA.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAONGEZEKA HADI ASILIMIA 5.5




Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo (kulia) akitoa taarifa ya mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Julai, 2016 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es salaam ambapo mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 mwezi uliopita kushoto ni Mtakwimu Bw. Opiyo mamu.
Waandishi wa Habari wakifatilia kwa makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ephraim Kwesigabo hayupo pichani akitoa taarifa ya mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Julai, 2016 leo Jijini Dar es salaam.PICHA NA ALLY DAUD-MAELEZO.

Na Ally Daud-Maelezo

Mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Juni, 2016 umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 mwezi uliopita kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephaim Kwesigabo amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kumesababishwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi.

“Mfumuko wa bei umesababishwa na kuongezeka kwa bei za vyakula kama vile mahindi ambayo yameongezeka kwa asilimia 3.2, unga wa muhogo kwa asilimia 2.4, samaki wabichi kwa asilimia 3.8, maziwa mgando kwa asilimia 4.3, maharage mabichi yaliyomenywa kwa asilimia 6.1, kitunguu swaumu kwa asilimia 12.5, njegere kwa asilimia 6.2, viazi mviringo kwa asilimia 2.5, mihogo mibichi kwa asilimia 6.7, magimbi kwa asilimia 4.5, na ndizi za kupika kwa asilimia 2.7,” amesema Kwesigabo.

Amesema bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na huduma ya kinywa na meno ambayo imeongezeka kwa asilimia 13.8, mafuta ya dizeli kwa asilimia 2.4 na mafuta ya petroli kwa asilimia 4.3. Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa mwezi Juni, 2016 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.5 ongezeko sawa na mwezi uliopita.

Aidha amesema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka wa bidhaa za vyakula majumbani na migahawani umeongezeka hadi asilimia 8.3 mwezi Juni, 2016 kutoka asilimia 7.2 mwezi Mei, 2016. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.47 mwezi Juni, 2016 kutoka 103.00 mwezi uliopita.

Kwesigabo amesema uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 96 na senti 65 mwezi Juni, 2016 kutoka mwezi Disemba, 2015.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Prof,Elisante Ole Gabrieli akutana na Wadau wa Utamaduni kutoka UNESCO

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(Katikati) akiongea na wadau wa utamaduni kutoka UNESCO  pamoja na Idara ya Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni katika  kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini,leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akimsikiliza Afisa Utamaduni kutoka UNESCO Bw.Louise Crayssac katika kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini,leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akimsikiliza Afisa Utamaduni kutoka UNESCO Bw.Halvor Storrusten katika kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akimsikiliza Afisa Utamaduni kutoka UNESCO Bi.Halvor Rehema Sudi katika kikao cha kujadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) akiwa katika picha na wageni kutoka UNESCO na Idara ya Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa baada ya kumalizika kikao kilichokuwa kikijadili mpango mkakati wa miaka mitano wa  maendeleo ya Utamaduni nchini,leo jinini Dar es Salaam.

RAIS MSTAAFU DK. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA NMB SABASABA




Meneja wa banda la Benki ya NMB katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016, Josephiner Kulwa (kushoto), akimkaribisha Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete alipotembelea banda hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
Hapa Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo.
Meneja wa banda la Benki ya NMB katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016, Josephiner Kulwa (kushoto), akitoa maelezo kwa Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete (katikati), akitoka katika banda la Benki ya NMB alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2016 yanayoendelea katika viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo . Kulia ni Meneja wa banda hilo, Josephiner Kulwa na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka. Maonesho hayo yatafikia tamati kesho kutwa.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA BANDA LA TTB SABASABA NA KUIPONGEZA KWA KAZI NZURI.




Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena (wa pili kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani moja ya majarida ya utalii ya TTB yaliyopo katika Banda la TTB.

Geofrey Meena, Meneja Masoko wa TTB akimwelezea Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Makani amna ambavyo TTB inavyotumia mbinu mbalimbali katika kutangaza vivutio vya Utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa TTB Bw. Philip Chitaunga(wa pili kulia ) akitoa maelezo kuhusu namna tuvuti maalumu ya Utalii (Online Tourism Portal) inavyofanya kazi na inavyoweza kutumiwa na wadau wa utalii kwa Naibu Waziri Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani huku afisa wa TTB Bw. Francis Malugu akisaidia kuonyesha kurasa za tovuti hiyo .

Naibu Waziri Eng. Ramo Makani akisisitiza jambo kuhusu tovuti maalumu ya Utalii baada ya kupata maelezo kuhusu tovuti hiyo kutoka kwa maafisa wa TTB.


Na: Geofrey Tengeneza

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani ameipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kazi nzuri inayoifanya katika kuitangaza Tanzania kama eneo bora la Utalii Duniani kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo tovuti maalumu ya utalii (Online Tourism Portal) na Nyenzo maalumu ya kutangaza utalii wa tanzania kupitia simu za mkononi ( Tanzania Tourism App).

Naibu Waziri huyo ametoa pongezi hizo alipotembelea Banda la Bodi ya Utalii Tanzania lililopo ndani ya jingo la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja vya Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

“ Kwa hakika mnafanya kazi nzuri sana katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii, endeleeni na juhudi hizo” alisema Naibu Waziri mara baada ya kupata maelezo mafupi kuhusu mbinu zinazotumiwa na TTB katika kuitangaza Tanzania kama eneo Bora la Utalii Duniani.
 
Blogger Templates