Pages

Ads 468x60px

Tuesday, January 12, 2016

MAJALIWA AENDA MHUMBILI KUMSALIMIA SUMAYE NA BALOZI KIBELLOH


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri Mkuu, Mstaafu Frederick Sumaye  ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu Januari 12, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amnaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa Matibabu Januari 12, 2016. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Esther Sumaye. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Balozi Hassan Kibelloh ambaye amelazwa katik hospitali ya taifa y Muhimbili kwa Matibabu Januari 12, 2016.

KILELE CHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana naRais Mstaafu wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo katika killele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 Pichani kutoka kushoto Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja zilizofanyika leo
 Baadhi ya Wananchi na Maafisa mbali mbali wa Serikali wakiwa katika sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaani Studium Mjini Unguja
  Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika Kilele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium zilizofanyika leo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium zilizofanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi walioshiriki katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo akiwa katika gari maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteremka katika gari maalum alilopanda wakati akiwasalimia wananchi katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo.

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA

 Waziri Ummy Mwalimu akisalimiana na Padri Lucius wa hospitali ya Peramiho Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Peramiho, Dr. Venance Mushi, alipotembelea hospitali hiyo asubuhi ya leo. Baadhi ya wanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), wakiwa sehemu ya mapokezi, tayari kwa kupata huduma.

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE ALIYELAZWA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye na Mama Esther Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 11, 2016
su1:Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Freredick Sumaye alipokwenda kumjulia hali katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Jumatatu Januari 11, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWAFARIJI FAMILIA YA NYERERE.

 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia  alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani. 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimfariji  na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,na wanafamilia  alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani. 
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani.

Sunday, January 10, 2016

David Kafulila na kesi mpya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma


Taarifa ninayokusogezea ni ya David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, tunafahamu ana kesi Mahakamani ya kupinga matokeo ya ubunge 2015 jimbo la Kigoma Kusini kesi ipo Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, taarifa ikufikie kuwa Kafulila baada ya kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma akasomewa kesi mpya ambayo anakiri hakuwa anaifahamu mwanzo kwenye sentensi zake; – David Kafulila
20150731001754
David Kafulila
‘Nilifikishwa mahakamani kwa kesi mpya ukiachilia kesi ya kwanza ya kupinga matokeo ya uchaguzi 2015 jimbo la Kigoma kusini, awali nilikuwa nikijua ninakesi moja katika mahakama ya hakimu mkazi kigoma kwa madai kwamba nilimdhalilisha aliyekuwa mkuu wa wilaya Khadija Nyembo tangu mwaka 2013….nikiwa mahakamani nikapewa tena kesi nyingine ni kesi ya kuhamasisha wananchi wasichangie mchango wa maabara; – David Kafulila
David-Kafulila1
‘Bado msimamo wagu utabaki palepale kwamba nitaendelea kupigania nchi yangu, kesi hizi zote katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma ukitazama hati za mashitaka yote ya Kafulila hapa Kigoma zimeandaliwa na kusainia na DPP makao makuu Dar es salam inawezekanaje;- Kafulila

Friday, January 8, 2016

UZINDUZI WA TAA ZA KUONGOZEA NDEGE KIWANJA CHA NDEGE PEMBA



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Zanzibar Kepten  Saidi Iddi Ndumbugani, kuhusu aina ya Taa mbali mbali zilizofungwa kwa uongozaji wa Ndege wakati wa ikitua  katika  sherehe ya uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Katika barabara ya ndege katika uwanja wa ndege wa Karume Pemba zikiwa zinaonekana Taa hizo zikiwa tayari kufanya kazi inayohitajiwa kwa wakati,taahizo zilizinduliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika  sherehe ya uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ngege Zanzibar Kepten  Saidi Iddi Ndumbugani, wakati alipofika kutembelea kuona  aina ya Taa mbali mbali zilizofungwa kwa uongozaji wa Ndege wakati wa ikitua  katika  sherehe ya uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Aina ya Taa zilizokuwa mwishoni mwa kiwanja cha ndege cha Karume Pemba zikiwa na Rangi ya Nyekundu na Buluu ambazo hutoa ishara kwa Kepteni anayeongoza Ndege ikitua,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbali aliofuatana nao walijionea  taa hizo namna zilivyofungwa  katika utaratibu maalum wakati  uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Aina ya Taa zilizokuwa nje kabisa ya  kiwanja cha ndege cha Karume Pemba  ambazo hutoa ishara kwa Kepteni anayeongoza Ndege ikitua,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbali aliofuatana nao walijionea  taa hizo namna zilivyofungwa  katika utaratibu maalum wakati  uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba uliofanyika jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kama iskara ya Uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha Ndege cha Karume Pemba jana ikiwa ni katika sherehe za shamra shamra za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar (kushoto) Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi(GAVU).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ngege Zanzibar Kepten  Saidi Iddi Ndumbugani, kuhusu majenereta yanayotoa umeme baada ya kuzindua rasmi  Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wafanyakazi Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na Wananchi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi wakati alipkuwa akitoa hutuba yake ya uzinduzi wa Taa za kuongozea Ndege kwenye kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk.Juma Malik Akili alipokuwa akitoa maelezo ya kitaalam kuhusu mradi wa uwekaji wa Taa  za kuongozea Ndege katika sherehe za uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi(GAVU) akitoa slamau za Wizara pamoja na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi katika sherehe za uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na wananchi katika sherehe za uzinduzi wa Taa za Kuongozea Ndege katika kiwanja cha ndege cha Pemba jana ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid na (kushoto) Naibu Waziri wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji

Thursday, January 7, 2016

Picha 11 za kushuhudia mzigo wa mvua za El Nino ulivyofunga barabara Marekani


Kama ulidhani mabalaa ya mafuriko huwa yanatokea Dar es Salaam pekeake au Tanzania pekeake, naomba nikwambie kwamba hilo lifute kichwani kwako !! Hata Marekani mzigo ukianguka wa kutosha, headlines za mafuriko lazima ukutane nazo.
Picha 11 hizi hapa, El Nino imeanguka Florida Marekani na hali haijawa mbaya eti kwa wanaoishi mabondeni pekeyako, mpaka barabara nazo zimefurika maji… imebidi mpaka barabara nyingine zifungwe kabisa.





FLO II
FLO III
FLO IV
Hapa ni uwanja wa ndege wa San Diego… maji yamejaa kwenye packing ya gari za kuchukulia abiria.
FLO V
Imebidi wengine wajaze mchanga kwenye mifuko kwa ajili ya kuzuia nyumba zisiingiliwe na maji… haya mambo hata Marekani yapo.
FLO IX
FLO VII
Tingatinga linasogeza kifusi kuzuia mawimbi ya bahari yasivuke na kuongezea balaa maeneo mengine.
FLO VIII
Hapo ni makazi ya watu, maji ya mafuriko yameondoka.. jamaa wanaendelea na usafi kutoa tope.
FLO X
Barabarani hali sio shwari, mti umeanguka kutokana na mvua na kufunga barabara.
FLO XI
Hapa limewekwa bango kuonesha barabara imefungwa.
FLO XII
Barabara ya juu iko salama kwenye flyover, lakini upande wa chini maji yamejaa.
FLO

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.

"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo" alisisitiza Jaji Warioba.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

07 Januari, 2016
 
Blogger Templates