CHUO
cha Kodi cha Mwenge jijini Dar es Salam wameitikia wito wa kauli ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Joseph Magufuli
kufanya usafi katika mazingira ya Chuo hicho.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Kodi, Edward Mwakimonga amewasihi wanafunzi pamoja na
wananchi kwa ujumla kuwa usafi ni afya na ikiwezekana iwe ni kawaida
kufanya usafi kila baada ya wiki mara moja ili kuweka mazingira safi.
Nae
Waziri Mkuu wa serikali ya chuo cha Kodi, Jeremia Shushu amewashukuru
wanafunzi pamoja na menejimenti ya chuo hicho kwa kukubali na kujitokeza
kwa wingi kushirikiana kufanya usafi katika mazingira ya chuo chao.
0 comments:
Post a Comment