WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la usafi lililofanyika leo nchini kote
lisiishie hapo bali liwe endelevu ili Tanzania iwe na taswira nzuri kwa wageni
wanaoingia nchini.Ametoa
wito huo leo (Jumatano, Desemba 9, 2015) kwenye soko la Kariakoo wakati
akishiriki zoezi la kufanya usafiikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John
Pombe Magufuli la kutaka maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru yasiwepo na badala
yake watu wote washiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi wa soko la Kariakoo wafike ofisini kwake
Jumatatu ijayo (Desemba 14, 2015) saa 4 asubuhi ili wamueleze wana mikakati
gani ya kuboresha utoaji huduma kwenye soko hilo.
"Natambua
kuwa siyo sahihi kupanga chini biashara tulizonazo. Nataka hawa viongozi waje
wanieleze wana mpango gani endelevu wa kuboresha soko hili," alisema
Waziri Mkuu huku akishangiliwa.Waziri
Mkuu ambaye alienda kufanya usafi kwenye soko hilo, alilazimika
kuzungumza na mamia ya wananchi waliofika kushiriki zoezi hilo. Pia alikagua
maeneo mbalimbali ya soko hilo hadi shimoni na kusema aneridhika na usafi
uliofanyika bali amesisitiza usafi huo uendelezwe.
"Kaulimbiu
ya Mheshimiwa Rais Magufuli ya HAPA KAZI TU inatupa ari ya kufanya kazi.
Fanyeni kazi. Watanzania mko huru kufanya kazi yoyote lakini cha msingi fuateni
taratibu na kanuni. Serikali hii tumamua kuwajali watu wa chini. Tutahakikisha
wajasiriamali wadogo, akinamama lishe na wamachinga mnafanya kazi kwa amani na
utulivu, " alisema.
Rais Magufuli
aliamua kuitangaza siku ya leo (Desemba 9, 2015) ambayo ni maadhimisho ya miaka
54 ya Uhuru iwe ni siku ya kufanya usafi nchi nzima ili kuepukana na magonjwa
mbalimbali na hasa kipindupindu.
0 comments:
Post a Comment