Pages

Ads 468x60px

Saturday, October 31, 2015

LEMBELI AELEZA HATMA YAKE BAADA YA KUUKOSA UBUNGE, AJIBU TETESI JUU YAKE IKIWEMO YA KUUZA REDIO YAKE


Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama Mjini, James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha Chadema.

Akiongea katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo hilo, Lembeli amesema kuwa hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.

Pia, Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.

Kadhalika, Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.

Kuhusu afya yake, alisema kuwa yeye ni mzima tofauti na habari zinazoendelea kuenea kuwa ni mgonjwa hasa baada ya kupata ajali ya gari na matokeo kutangazwa.

TAARIFA YA ZADIA KUHUSU KUFUTWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI ZANZIBAR.



Logo ya Zadia
Jumuiya ya Wazanzibari Waishio Nchini Marekani (ZADIA), imekuwa ikifuatilia kwa karibu na makini zaidi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa mchakato wa uchaguzi ulifanyika kwa njia za amani na utulivu.
 Hata hivyo ZADIA imeshtushwa mno na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Jecha Salim Jecha la kutangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake.
Ama kwa hakika kitendo hicho hakikuwa cha busara na kinapelekea kurudisha nyuma maendeleao ya demokrasia Zanzibar, na vilevile hakiashirii mustakbali mwema kwa nchi yetu tuipendayo. 
Wazanzibari wameelezea maoni na matakwa yao kwenye visanduku vya kupigia kura, na maoni na matakwa yao hayo yanapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa.
Kwa hivyo, ZADIA inatoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, kumalizia mchakato mzima wa kuhesabu kura kwa majimbo yaliyobakia na kutoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi na kumtangaza mshindi ili kuiepusha Zanzibar yetu tuipendayo kuingia katika hali ya mtafaruku na mifarakano isiyokuwa na tija bali kuleta hasara.
ZADIA pia inaungana na jumuiya zote za kimataifa ambazo zimetoa msimamo wao juu ya uchaguzi wa Zanzibar, hasa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ambao ni kiungo madhubuti kati ya Wazanzibari walioko Zanzibar na wenzao wanaoishi nchini Marekani.
Aidha, tunapenda kumkumbusha Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dakta Ali Mohammed Shein kuwa Wazanzibari walimpa amana kubwa ya kuwaongoza, na kwa hivyo ni wajibu wake kuienzi amana hiyo kwa kuchukuwa hatua za kiungwana za kuitoa Zanzibar kwenye mgando huu wa kisiasa. Hali hii iliyopo sasa inaleta wasiwasi miongoni mwa raia na imekua ikiathiri maisha yao ya kila siku, na ikiachwa kuendelea huenda ikaathiri pia mustakbali maisha yao kwa jumla.
ZADIA pia inamtolea wito Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake aliyonayo kuhakikisha Zanzibar inatoka kwenye mkwamo huu wa kisiasa na kwamba anaondoka madarakani akiiacha Zanzibar ikiwa katika hali ya amani na utulivu. Kwa kufanya hivyo atauthibitishia ulimwengu kuwa kweli Tanzania ni kisima cha amani.
Na mwisho tunawaomba Wazanzibari, wapenzi wa Zanzibar, na Watanzania wote kwa ujumla popote pale walipo, wajitahidi kufanya mawasiliano na Jumuiya nyengine za Kimataifa ili ziingilie kati suala hili kabla nchi yetu haijaingia kwenye mtafaruku mkubwa wa kisiasa na kijamii na hata kupelekea kuhatarisha amani ya nchi yetu.
Mungu Ibariki, Zanzibar.

RAIS DK.JAKAYA KIKWETE AZINDUA KAMPUNI YA SOKO LA BIDHAA KUSAIDIA WAKULIMA NCHINI

02
Rais Dk.Jakaya Kikiwete akizundua kampuni ya Soko la Bidhaa  katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
05 
Rais Dk.Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na Bodi ya Kampuni ya Soko la Bidhaa wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
01
Rais Dk.Jakaya Kikwete akizungumza wakati uzinduzi wa Kampuni ya Soko la Bidhaa iliyofanyika katikza ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam Oktoba 30, 2015.
03
Waziri wa Fedha na Uchumi,Saada Mkuya akizungumza na wakati uzinduzi wa kampuni ya Soko la bidhaa  jijini Dar es Salaam.
04
Sehemu wataalam mbalimbali wakiwa wamekekti katika uzinduzi wa Kampuni ya Soko la Bidhaa  jijini Dar es Salaam.



Rais Dk.Jakaya Kikwete amesema kuanza kwa kampuni ya soko la bidhaa kutasaidia wakulima kupata soko la uhakika na kukuza uchumi pamoja na kupata bima katika kilimo.
  Hayo ameyasema leo wakati uzinduzi wa Kampuni ya soko la bidhaa jijini Dar es Salaam,Dk.Kikwete amesema wakulima wamekuwa wakilima lakini masoko yao hayana uhakika na kilimo hakina tija.
  Amesema kuwa mfumo utasaidia wakulima kupata bei ya uhakika wa kuuza mazao yao na wanunuzi kufahamu bei ya soko la bidhaa wanayoihitaji. Dk.Kikwete ameitaka watu wanaofanya kazi kuwa waaminifu katika kuweza kuwafanya wakulima wanufaike na soko hilo kwa kuwaletea maendeleo ya kuendeleza na kuachana na kutafuta masoko ambayo mwisho wa siku wanauza kwa hasara.
  Aidha amesema soko la bidhaa litawaondolea wakulima ukopwaji ambao umekuwa ukiwakatisha tamaa na kushindwa kuendeleza kilimo chenye tija. Amesema wakulima wamekuwa wakifanya kazi zao za kilimo wakiwa na changamoto kubwa ya kukosa soko la uhakika na kufanya mazao kununuliwa na watu wachache kwa bei ya chini.
  Dk.Kikwete amesema wakulima wakiwa wana soko la uhakika kutafanya waweze kuingia katika bima kutokana na kilimo kuonyesha mwanga katika sekta hiyo.Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Soko la Bidhaa (TMX),Nasama Masinda amesema kuwa soko hilo wataanzia mazao ya Ufuta,Korosho pamoja na mpunga .
  Amesema wamejipanga katika kuhakikisha wanaweka uwazi wa soko katika bidhaa hizo kwa wanunuzi na wauzaji kuwa na bei inayoendana na soko.

MAGUFULI AWASHUKURU WAPIGA KURA


 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wapenzi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla fupi ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa uliofanyika oktoba 25 mwaka 2015. 
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia)akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana(katikati) pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakati wa sherehe ndogo ya kushukuru wapiga kura walioipa CCM ushindi.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote
waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba
ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kwa  wananchi waliojitokeza kumpongeza nje ya Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akionyesha cheti alichokabidhiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kushinda kiti cha Urais kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015.
 Mama Samia Suluhu aliyekuwa Mgombea Mwenza akionyesha cheti chake cha Umakamu wa Rais kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mke wake Janeth Magufuli mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mteule wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza kwenye hafla hiyo ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya Ofisi Ndogo CCM Lumumba.
 Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa jiji la Dar es Salaam mara baada ya kumalizika hafla ya kuwasalimu na kuwashukuru kwa kumpigia kura zilizompa ushindi wa kiti cha Urais.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya ofisi ndogo CCM Lumumba.

KIWIA AKANUSHA KUZIMIA BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA. ASEMA ANATARAJIA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI KWANI BADO HAJASAINI MATOKEO.


Highness Kiwia akionyesha moja ya karatasi yenye makosa
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi Ukawa Highness Kiwia, anatarajia kufungua kesia ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimboni humo kwa madai kwamba haukuwa wa huru na haki kutokana na kugubikwa na changamoto mbalimbali.

Kiwia ambae ameshindwa kutetea jimbo hilo baada kuchukuliwa na Angelina Mabula kutoka Chama cha Mapinduzi CCM, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na Uchaguzi huo.

Alieleza kuwa katika vituo mbalimbali jimboni humo kulikuwa na makosa mengi ambayo ni pamoja na uwepo wa vituo hewa, idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kupigia kura pamoja na majina ya wapiga kura kukutwa katika majimbo tofauti na yale waliyojiandikishia.

Katika hatua nyingine Kiwia alikanusha taarifa kuwa alimtuma mwakilishi kwa ajili ya kusaini fomu ya matokeo kwa niaba yake na kwamba siku ya kutangaza matokeo alishindwa kupokea matokeo hayo na hivyo kuzilai.

Kwa upande wake Tungaraza Njugu ambae ni Kiongozi wa Kanda ya Ziwa Victoria Chadema, alisema kuwa zoezi la uchaguzi mwaka huu linapaswa kulaaniwa kwa kuwa halikuendeshwa kidemokrasia kutokana na kukiuka taratibu mbalimbali za uchaguzi.

Katika Matokeo ya Kiti cha Ubunge Jimboni Ilemela, Mgombea wa CCM Angelina Mabula aliibuka mshindi baada ya kupata kura 85,424 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema Highness Kiwia aliepata kura 61,679 ambapo kwa upande wa Madiwani CCM ilishinda Kata 16 huku Kata Tatu zikichukuliwa na upinzani.
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema
Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chadema akiongea na wanahabari

Friday, October 30, 2015

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI WA URAIS WA TANZANIA AWAMU YA TANO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi cheti cha Urais Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu wa Rais Mteule, Samia Hassan Suluhu.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia), akimkabidhi cheti cha Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu katika hafla hiyo.
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kulia), akiwapungia mkono wananchi wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa cheti cha urais. Kutoka  kushoto ni mgombea urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha ADC, Chief Lutalosa Yemba.
 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto), akimpongeza Rais Mteule wa Tanzania Dk. John Magufuli baada ya kuchaguliwa kuwa rais.
 Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakishangilia wakati Rais Mteule wa Tanzania Dk.John Magufuli alipokuwa akitoka Ukumbi wa Diamond Jubilee kukabidhiwa cheti cha urais.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Magufuli akimuonesha Rais Jakaya Kikwete cheti cha ushindi.
 Rais Mteule wa Tanzania, Dk.Makufuli akiwa katika picha ya pamoja na wagombea urais wenzake wa vyama vingine.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva kwa kusimamia vizuri uchaguzi mkuu wa 2015.
Rais Jakaya Kikwete na Rais Mteule Dk.John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wake zao kwenye hafla hiyo.

Magufuli akabidhiwa Hati ya Ushindi Nafasi ya Urais

Rais mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli akionesha cheti chake cha ushindi alichokabidhiwa muda huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee



Na Anitha Jonas na Beatrice Lyimo- MAELEZO.
 
Watanzania wametakiwa kukubaliana na matokeo ya  Uchaguzi Mkuu  wa mwaka 2015, yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kwa kuwa  ni ya haki na hakuna aliyeibiwa kura.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Waangalizi wa Uchaguzi kutoka nchi za Jumuiya ya Madola nchini na ambaye Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodlucky Jonathan kwenye halfa ya kumkabidhi hati Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika  leo kwenye ukumbi wa Diamond  Jubilee  jijini Dar es salaam.

“Uchaguzi ulikuwa wa haki na amani na hakuna yeyote aliyeibiwa haki yake kwani matokeo hayo yamedhibitishwa kuwa ya uhuru na haki kwa kufuata misingi ya sheria na taratibu zilizopo” alisema  Rais Mstaafu Jonathan.

Kwa upande wa mgombea urais kupitia chama cha ACT wazalendo Bibi. Anna Mghwira amesema kuwa chama chake kimemkubali matokeo ya uchaguzi uliompitisha Dkt. John Magufuli.

Vilevile ameongeza kuwa wagombea wote walizungumza kuhusu mabadiliko hivyo ana imani na mshindi wa nafasi hii atalisimamia ipasavyo.

“Watanzania wanahitaji mabadiliko hasa katika Katiba Mpya itakayotokana na maoni ya Watanzania, kuimarisha umoja wa kimataifa, kuinua uchumi wa nchi, kusimamia shughuli za Serikali pamoja na kuboresha usawa wa kijinsia kati ya mwanamke na mwanamume,” aliongeza Bibi Mghwira.

Mbali na hayo mgombea huyo wa urais kupitia chama cha ACT wazalendo amemkabidhi Rais Mteule Ilani ya chama hicho kama muongozo kwa yale yaliyopungua katika Ilani ya cha chake.

Aidha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewapongeza wananchi kwa kuwa na mwamko mkubwa wa kupiga kura na kuliendesha zoezi hilo kwa amani.

Pia Jaji Mstaafu Lubuva alimkabidhi hati ya ushindi mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi.

KIKWETE AMPONGEZA DK MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015

Rais Kikwete akimsomea Magufuli sms za pongezi kutoka kila pembe ya dunia.

Mkono wa Pongezi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.

Dk John Pombe Magufuli akipokea simu moja wapo za pongezi kutoka kwa Mgombea wa ACT Wazalendo, Anna Mgwira.

Mazungumzo na vicheko vya furaha vikiendelea

Thursday, October 29, 2015

Kuanzia wa kwanza mpaka wa mwisho… asilimia mpaka idadi ya kura za matokeo yote ya Urais 2015 Tanzania



Dr. John Pombe Magufuli wa (CCM) ametangazwa mshindi wa kiti cha urais kutoka kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 ambapo ameongoza kwa zaidi ya asilimia 50, matokeo kamili ndio haya hapa chini.

BREAKING: Dr. Magufuli ametangazwa mshindi kiti cha Urais Tanzania, list yote na asilimia viko hapa



October 29 2015 ndio siku yenyewe matokeo ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 yametangazwa ambapo Dr. John Pombe Magufuli (CCM) ndio ametangazwa mshindi akiongoza kwa asilimia 58, anaemfatia ni Edward Lowassa akiwa na asilimia 39.
Aliyeshika nafasi ya tatu ni mama Anna wa ACT aliyepata 0.65%, huku Chief Yemba wa ADC akipata 0.43%, wa tano ni Hashim Rungwe wa CHAUMMA 0.32%, huku NRA, TLP na UPDP wakipata wote asilimia 0.05.

Maneno ya kwanza ya Profesa Jay baada ya kushinda kiti cha Ubunge





Bado tupo kwenye headlines za uchaguzi 2015 ambapo msanii mkongwe wa HipHop Tanzania Joseph Haule (Profesa Jay) ni mmoja wa wawashindi wa kiti cha ubunge kwenye uchaguzi huu akiwa amechukua jimbo la Mikumi Morogoro na anachosubiri kwa sasa ni kuingia bungeni.
Prof. ameongea na millardayo.com >>>‘Nawashukuru sana wananchi wa Mikumi kwa kuniamini na kunipa dhamana hii kubwa, watanzania wameniamini kwa sababu ya upeo mkubwa ambao Mungu amenipa, naamini sana katika umoja na mshikamano….! na ndiomaana nimekuwa nasisitiza hata katika kampeni zangu, lazima tushikamane watu wote wa vyama vyote na hata wasio na vyama ili kuikomboa Mikumi yetu ‘ –
.
.
‘Changamoto kubwa ni maji, elimu, miundo mbinu pamoja na ajira, nitaendelea kuwatumikia wananchi wangu kwasababu wao ndio wamenituma Dodoma, mimi kuwa mwanamuziki halitonizuia kuwawakilisha wananchi…. nitaendelea kuwa mwanamuziki na huwenda nikafanya muziki ule wa juu zaidi kwasababu nategemea kukutana na watu wa juu zaidi’– PROFESSOR J
prof
Unaweza ukabonyeza play hapa chini kumsikiliza Professor Jay akizungumza kuhusu ushindi wake wa kiti cha Ubunge

DUNI AZUIWA KUWASILISHA HATI YA PINGAMIZI YA MATOKEO JIJINI DAR LEO.

Mgombea mwenza wa CHADEMA Juma Duni Haji amezuiwa kuingia katika chumba cha kutangazia matokeo ya urais katika ukumbi wa Julius Nyerere wakati zoezi hilo likiendelea baada ya kueleza kuwa ameleta hati ya pingamizi ya matokeo.

Hata hivyo walinzi wa eneo la kutangazia matokeo walimkatalia kuingia katika chumba hicho na kumtaka aende Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchguzi (NEC) kuwasilisha hati yake hiyo na kisha kusindikizwa kwenye gari alilokuja nalo lenye namba T754 DDY aina ya Toyota.

Wednesday, October 28, 2015

Rais Kikwete apokea hati za Utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne

JA1
Balozi mpya wa Misri hapa nchini Mhe.Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf wakiwalisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kikwete ikulu jijini Dar Es Salam leo.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanaziwakilisha nchi zao hapa Tanzania.Mabalozi waliowasilisha hati zao kwa Rais Kikwete ikulu asubuhi ya leo ni pamoja Mhe.Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf Balozi mpya wa Misri hapa nchini, Mhe.Yahel Vilan Balozi mpya wa Israel nchini Tanzania, Mhe.Bayani Mangibin balozi mpya wa Ufilipino nchini na Mhe. Tan Puay Hiang Balozi mpya wa Singapore nchini Tanzania.Pichani Mabalozi hao wakiwasilisha hati zao za utambulisho.
JA2
-Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambusho kutoka kwa Mhe.Yahel Vilan Balozi mpya wa Israel hapa nchini,
JA3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa mhe.Bayani Mangibin Balozi mpya wa Ufilipino nchini Tanzania.
JA4
-Balozi mpya wa Singapore nchini Tanzania Mhe.Tan Puay Hiang akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam
 
Blogger Templates