Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya nchini umekanusha kuwepo kwa madai
yaliyotolewa na Hospital ya Rufaa Mkoani Mbeya kuwa wanaudai Mfuko
jumla ya shilingi bilioni 2 na kwamba wanaudai Mfuko kutoka mwezi Juni,
2015.
Akizungumza
jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Ndugu Michael Mhando amesema madai yaliyotolewa na Hospitali hiyo ya
Rufaa Mkoa wa Mbeya hayana ukweli wowote nakwamba mfuko huo unalipa
madai baada ya mtoa huduma kuwasilisha kwenye Mfuko.
Amesema
madai ya mwisho ya Hospitali hiyo kulipwa ni ya mwezi Agosti, 2015.
Madai ya mwezi Septemba, 2015 yamewasilishwa kwenye Mfuko Novemba 4,2015
ambayo mpaka sasa yana siku 15 tu. Kwa hiyo Hospitali ya Rufaa ya Mbeya
tumewalipa madai yao yote na kwa mwaka huu wa 2015 kuanzia Januari hadi
Agosti 2015 tumewalipa kiasi cha shilingi bilioni 4.3.
Madai
mengi ambayo yamekuwa yakiwasilishwa kwao yamegubikwa na udanganyifu
mkubwa hali inayowafanya kuchukua muda mrefu katika uhakiki wake ikiwemo
kuwapigia simu wagonjwa waliopewa huduma za matibabu.
Aidha
Mhando amesema mfuko huo unatoa onyo kali kwa watoa huduma ambao
wamekuwa bado wakijihusisha na udanganyifu wa aina yoyote kwa kuwa
haitawaonea haya kuwafutia usajili na kuwafikisha katika vyombo vya
sheria.
Amesema
Mfuko pia unazidi kutoa rai kwa watoa huduma kutumia fursa zinazotolewa
na Mfuko katika kuhakikisha huduma za matibabu zinaboreshwa kwa
wanachama na Watanzania kwa ujumla.
Wakati
huo Kaimu mkurugenzi huyo amesema Katika kipindi hiki, baadhi ya watoa
huduma wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali za kushindwa kutoa huduma
nzuri ama za kuridhisha kwa wanachama wao na wananchi kwa ujumla kwa
kisingizio cha kukosa fedha hali inayosababisha kukosa dawa, kukosa
vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kushindwa kuboresha mazingira ya
vituo.
Watoa
huduma hao wanadai hayo ama wanatoa visingizio vya kukwama huduma
katika maeneo yao kutokana na NHIF kuchelewa kulipa fedha fedha za madai
ambayo wametibia wanachama wake.
Amesema
taarifa hizo zinajenga mazingira kuwa NHIF ni kikwazo katika ufanisi
wa vituo hivyo jambo ambalo si la kweli na limebeba taswira ya kuleta
chuki baina ya wanachama ama wananchi na chombo chao ambacho kina
dhamana ya kuwatibia.
Hata
hivyo Mhando amekanusha kuwa wao ndio kikwazo ama sababisho la huduma
mbovu katika vituo hivyo nah ii inatokana na ukweli kwamba zipo jitihada
mbalimbali ambazo NHIF imekuwa ikizifanya kuhakikisha inasaidiana na
Serikali katika kuboresha huduma za vituo hivyo ili wananchi kwa pamoja
wapate huduma zinazostahili.
0 comments:
Post a Comment