
Chama
 cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimesitisha shughuli za mazishi ya 
aliekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani Geita marehemu Alphonce 
Mawazo, baada ya jeshi la polisi Mkoani Mwanza kuzuia zoezi la kuuaga 
mwili wake lililokuwa limepangwa kufanyika juzi jumamosi Jijini Mwanza. 
Mwenyekiti
 wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe alibainisha hayo jana wakati 
akizungumza na Wanahabari Mkoani Mwanza, ili kutoa msimamo wa Chama 
baada ya kuwepo kwa mazungumzo baina yake na familia ya marehemu 
Mawazo. 
Alisema
 kuwa baada ya mazungumzo hayo, Chadema pamoja na familia ya marehemu 
Mawazo wamekubaliana kwenda Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kufungua shauri
 la kuomba tafsiri ya Kimahakama juu ya zuio hilo la jeshi la polisi 
kuzuia mwili wa marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza kabla ya Kwenda 
kuzikwa Kijijini kwake Chikobe katika Wilaya ya Busanda Mkoani Geita.
Nae
 Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mlezi wa marehemu Mawazo, 
alisema anasikitishwa na hatua iliyochukuliwa na jeshi la polisi ya 
kuzuia mwili wa marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza ambapo ameeleza 
kuwa na matumaini makubwa ya kwamba mahakama itatenda haki juu ya suala 
hilo.
Frederick
 Sumaye pamoja na Edward Lowasa ambao ni Viongozi Waandamizi wa Chadema,
 walisema hatua ya jeshi la polisi kuzuia mwili wa Mawazo kuagwa Jijini 
Mwanza si sawa na kwamba inaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani. 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment