Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
 Mfuko
 wa Taifa wa Bima ya Afya nchini umekanusha kuwepo kwa madai 
yaliyotolewa na Hospital ya Rufaa  Mkoani Mbeya kuwa  wanaudai Mfuko 
jumla ya shilingi bilioni 2 na kwamba wanaudai Mfuko kutoka mwezi Juni, 
2015.
Akizungumza
 jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya 
 Ndugu Michael Mhando amesema madai yaliyotolewa na Hospitali hiyo ya 
Rufaa Mkoa wa Mbeya  hayana ukweli wowote nakwamba mfuko huo  unalipa 
madai baada ya mtoa huduma kuwasilisha kwenye Mfuko.
Amesema
 madai   ya mwisho ya Hospitali hiyo kulipwa ni ya mwezi Agosti, 2015. 
Madai ya mwezi Septemba, 2015 yamewasilishwa kwenye Mfuko Novemba 4,2015
 ambayo mpaka sasa yana siku 15 tu. Kwa hiyo Hospitali ya Rufaa ya Mbeya
 tumewalipa madai yao yote na kwa mwaka huu wa 2015 kuanzia Januari hadi
 Agosti 2015 tumewalipa kiasi cha shilingi bilioni 4.3.
Madai
 mengi ambayo yamekuwa yakiwasilishwa kwao yamegubikwa na udanganyifu 
mkubwa hali inayowafanya kuchukua muda mrefu katika uhakiki wake ikiwemo
 kuwapigia simu wagonjwa waliopewa huduma za matibabu.
Aidha
 Mhando amesema mfuko huo unatoa onyo kali kwa watoa huduma ambao 
wamekuwa bado wakijihusisha na udanganyifu wa aina yoyote kwa kuwa 
haitawaonea haya kuwafutia usajili na kuwafikisha katika vyombo vya 
sheria.
Amesema
 Mfuko pia unazidi kutoa rai kwa watoa huduma kutumia fursa zinazotolewa
 na Mfuko katika kuhakikisha huduma za matibabu zinaboreshwa kwa 
wanachama na Watanzania kwa ujumla.
 Wakati
 huo Kaimu mkurugenzi huyo amesema Katika kipindi hiki, baadhi ya watoa 
huduma wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali za kushindwa kutoa huduma 
nzuri ama za kuridhisha kwa wanachama wao  na wananchi kwa ujumla kwa 
kisingizio cha kukosa fedha hali inayosababisha kukosa dawa, kukosa 
vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kushindwa kuboresha mazingira ya 
vituo.
Watoa
 huduma hao wanadai hayo ama wanatoa visingizio vya kukwama huduma 
katika maeneo yao kutokana na NHIF kuchelewa kulipa fedha fedha za madai
 ambayo wametibia wanachama wake.
Amesema
 taarifa  hizo zinajenga mazingira kuwa NHIF ni kikwazo katika ufanisi 
wa vituo hivyo jambo ambalo si la kweli na limebeba taswira ya kuleta 
chuki baina ya wanachama ama wananchi na chombo chao ambacho kina 
dhamana ya kuwatibia.
Hata
 hivyo Mhando amekanusha kuwa wao  ndio kikwazo ama sababisho la huduma 
mbovu katika vituo hivyo nah ii inatokana na ukweli kwamba zipo jitihada
 mbalimbali ambazo NHIF imekuwa ikizifanya kuhakikisha inasaidiana na 
Serikali katika kuboresha huduma za vituo hivyo ili wananchi kwa pamoja 
wapate huduma zinazostahili.
 
 
 
 
 
 

 
 
0 comments:
Post a Comment