Meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na kijana Innocent Aloyce baada ya kumkabidhi zawadi ya Toyo, alipomtembelea katika shamba lake
mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” kwa nyanja mbalimbali miezi sita iliyopita.
Meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael (kushoto) akimwangalia kijana Innocent Aloyce baada ya kumtembelea katika shamba lake mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi ambaye ni
miongoni mwa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” kwa nyanja mbalimbali miezi sita iliyopita.
Meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na kijana Innocent Aloyce baada ya kumkabidhi zawadi ya Toyo, alipomtembelea katika shamba lake
mkoani Mwanza wilaya ya Misungwi ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” kwa nyanja mbalimbali miezi sita iliyopita huku akishuhudiwa na ndugu na wafanyakazi wa Airtel.
Jijini Mwanza Wilaya ya Misungwi, kampuni ya Airtel kupitia mradi wake wa *Airtel Fursa Tunakuwezesha imefurahishwa na juhudi zilizoonyeshwa na kijana Innocent
Aloyce mkaazi wa kijiji cha Mwalogwabagole ambaye ameonyesha
mafanikio katika shughuli zake za ulimaji mbogamboga na nyanya tangu kupatiwa mashine ya kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji pamoja na jembe la plau miezi mitatu iliopita.
Airtel kupitia mradi wake wa Airtel Fursa Tunakuwezesha, umeendelea
kuwawezesha zaidi vijana uliowashika mkono, wanaozidi kuonyesha mafanikio katika kuboresha shughuli zao mbalimbali za kijasiriamali.Ikiwa na lengo la kuwakwamua vijana kiuchumi na kujiajiri wao wenjewe ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira .
Akielezea changamoto za usafirishaji wa mazao yake mjasiliamali huyu
ameeleza tofauti anayoiona mara baada ya kukabidhiwa chombo cha
usafirishaji mazao kutoka kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel
walipomtembelea shambani kwake mwishoni mwa wiki hii na kuona maendeleo yake ya shughuli zake za ulimaji.
Katika kukabidhi pikipiki kwa ajili ya usafirishaji mazao kwa Innocent,
meneja masoko wa kampuni ya Airtel kanda ya Ziwa, Emmanuel Raphael
amewataka vijana kuiga mfano unaaonyeshwa na Innocent.
Aliongeza kwa kusema “vijana inabidi waachane na dhamira ya kutaka kukaa tu vijiweni na kusubiri watafutiwe ajira. Ni juhu di zao wao wenyewe ndio zitakazoweza kuwakomboa na kupata maendeleo kama alivyoweza kufanikiwa Innocent.
Kufuatia kushikwa kwake mkono na Airtel leo hii Innocent meweza
kubadilisha maisha yake na familia yake. Hiyo nawahimiza vijana wasikate
tamaa na kujitokeza kwa wingi kwa kuchangamkia fursa hii na nyingine nyingi
zinazowazunguka”, .
0 comments:
Post a Comment