Mh.
Prof. Mbarawa akiongea na menejimenti ya Dawasco na Dawassa kwenye
ukumbi wa Dawasco gerezani,mwishoni mwa wiki jijini Dar.(picha na
Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii) .
Mh.
Prof. Makame Mbarawa akisaini kitabu cha wageni akiwa na Naibu
waziri,Injinia Isack Kamwelwe (kushoto), pamoja na katibu mkuu na naibu
katibu mkuu wa wizara ya maji (kulia) katika ofisi ya afisa mtendaji
mkuu wa Dawasco.
Waziri wa maji mh. Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Dawasco mapema leo alipotembelea makao makuu ya ofisi hizo
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasco Injinia Cyprian Luhemeja akiwa na waziri wa
maji Prof. Makame Mbarawa mara tu baada ya kuwasili katika ofisi hizo
Shirika
la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco) limetakiwa kuongeza
idadi ya wananchi wanaopata Maji jijini Dar es salaam kutoka wateja
148,000 waliopo sasa hadi wateja milioni 1 ifikapo Juni 2016.
Akiongea
na Menejimenti ya Dawasco na Dawasa ikiwa ni siku moja tangu
kuchaguliwa kwake Waziri wa Maji Mh. Prof Makame Mbarawa alizitaka
Taasisi hizo kuweka mkakati wa lazima utakao hakikisha wateja milioni
wanaunganishwa kwenye mtandao wa Majisafi na salama kwa wakazi wote
jijini.
“Tumekuja
kutekeleza ahadi ya Rais Magufuli aliyoitoa bungeni kuhusu Maji.
Aliahidi Serikali ya awamu ya tano pamoja na mambo mengine watahakikisha
wana mtua Mama ndoo kichwani” alisema Mh Waziri.
Aliongeza
kuwa lazima taasisi hizi mbili zijue wajibu wake kwa wananchi na
kutekeleza ahadi ya Rais ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa kutafuta
Maji na hata wakiyapata gharama zisiwe juu, ameitaka Dawasco kuhakikisha
inawahimiza wateja wake wote na taasisi za serikali kulipia Ankara za
Maji kwa wakati.
Aidha
amewahimiza Dawasa kuboresha mtandao wa Majitaka ili kuwafikia wateja
wengi zaidi wanaohitaji huduma hiyo ya Majitaka na kuepusha usumbufu kwa
wananchi unaotokana na Majitaka hayo kuendelea kumwagika ovyo katika
mitaa mingi ya jiji.“Hakikisheni mnaboresha mfumo wote wa Majitaka,
uendane na mahitaji ya sasa ya jiji ili kuwapunguzia wananchi kupata
kero mbalimbali zinazotokana na uchavu wa miundombinu ya Majitaka”
alisema Mh.Mbarawa.
0 comments:
Post a Comment