Waziri
wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akiangalia Ng'ombe walio
uwawa katika Mgogoro wa wakulima na Wafugaji uliotokea katika kijiji cha
Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero, katika tukio lililotokea
Desemba 12 mwaka huu.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akiwa na Mkuu
wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa wakiwajulia hali watu waliojeruhiwa
katika mgogoro wa wakulima na wafugaji uliotokea katika kijiji cha
Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero Desemba 12 mwaka huu.
Waziri
wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akizungumza na Mkuu wa
wilaya Mvomero, Betty Mkwasa katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga
wilayani Mvomero Desemba 12 mwaka huu, walipotembelea katika kijiji
hicho na kuona madhara makubwa yaliyojitokeza katika mgogoro wa wakulima
na wafugaji. Nchemba alimwagiza Mkuu wa wilaya Mvomero, Beth Mkwasa
kuunda kamati ya Ulinzi na Usalama katika wilaya ya Mvomero ili kamati
ihusike maeneo yote ya Nchi yetu ili kuhakikisha wanaimarisha ulinzi
maeneo yote yenye migogoro, pia wahakikishe waliosababisha maafa
wanakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akizungumza na
wanachi wa kijiji cha Dihinda waliokusanyika katika eneo lililotokea
mauaji ya wanyama na baadhi ya watu kujeruhiwa.
"Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima,
kuwa hakuna ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu
yeyote yule, njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha
wakuliama na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa
Serikali wa eneo husika hatua kwa hatua, Nawaomba wananchi waache
kujichukulia sheria mikononi, tunakwenda kuunda kamati za usuruhishi wa
migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili
kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria." Alisema
Nchemba.



0 comments:
Post a Comment